Na Oscar Assenga, Tanga.
TIMU ya Kilimani FC ya Zanzibar na Coastal Union U-20 juzi
zilishindwa kutambiana baada ya kufungana bao 1-1, katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika jana kwenye uwanja wa mkwakwani mjini hapa.
Mchezo huo ulikuwa ni miongoni mwa michezo ya maandalizi kwa timu ya Kilimani FC ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza visiwani humo kabla ya kuanza msimu mpya.
Timu hiyo ipo mkoani Tanga katika ziara ya kimichezo kwa
michezo minne lengo lao likiwa ni kuimarisha undugu kwa timu watakazo cheza nazo
wakiwa mkoani hapa kabla ya kuondoka kwenda Mombasa ambapo watacheza mechi
nyengine za kirafiki.
Kocha wa timu Kilimani FC ,Bakari Mchunga alisema baada ya
kumalizika mechi hiyo ya juzi wataelekea Duga Stars wilayani Mkinga na kuelekea
Mombasa kucheza na timu ya Dunga ya Msambweni pamoja na timu ya Nzuri ya Kenya
na baadae kurejea mkoani hapa kwenda Maramba wilayani Mkinga kucheza mechi moja
ya kirafiki.
Kwa upande wake,Kocha wa timu ya U-20 Coastal Union,Joseph Lazaro alisema mchezo huo ulikuwa ni kukipa makali kikosi hicho ambacho kinajiandaa na msimu mpya wa mashindano ya vijana.
EmoticonEmoticon