Odula atua Coastal Union.

July 15, 2013
(Picha juu ni Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim El Siagi aliyevaa shati jeupe na mistari meusi akizungumza na mmiliki wa Blog hii kuhusu ujio wa mchezaji huyo ambao utaleta ushindani mkubwa sana)

Na Oscar Assenga,Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema tayari umeshamalizana na aliyekuwa mshambulizi wa timu ya Bandari ya Kenya,Christian Odula kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea timu kwenye msimu mpya ambao utaanza Agosti mwaka huu.

Akizungumza na Blog hii,Katibu Mkuu wa timu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim El Siagi alisema baada ya kumalizina na mchezaji huyo anatarajiwa kutua mkoani Tanga wiki ya leo akiwa na mchezaji mwengine wa timu hiyo Jerry Santos.

Siagi alisema msimu huu wamedhamiri kufanya usajili wa nguvu ambao utaifanya timu hiyo kuwa tishio kwenye mechi zao za Ligi kuu ya Tanzania bara kwani malengo yao ni kuchukua ubingwa wa mashindano hayo makubwa hapa nchini.

Aidha alisema timu hiyo itacheza mechi mbalimbali za majaribio nchini Kenya na timu za Sofapaka,Bandari na Goromahia lengo likiwa ni kukipa makali kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kuwa tishio.

Katibu huyo aliwataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuendelea kujitokeza kuisapoti timu hiyo ili iweze kutimiza azma yao waliyojiwekea kwenye michuano hiyo.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »