MBUNGE wa Jimbo la Tanga,Omari Nundu ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kuangalia uwezekano wa kuvirudisha viwanda vilivyokufa mkoani hapa ili viweze kurudi katika hali yake kama ilivyokuwa hapo zamani.
Kauli ya Mbunge huyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa mradi wa Tanga Economic Corridor Limited uliofanywa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Ghali Bilal ambapo amesema mradi huo mkubwa mkoa utabadilika kutokana na uwepo wa viwanda 17 ambavyo
vinatarajiwa kujengwa katika eneo la Pongwe jijini Tanga.
Nundu amesema mradi huo utakapokamilika utawasaidia wananchi kuweza kupata ajira pamoja na kuzalisha fuksa mbalimbali hali ambayo itasaidia kuwaondolea umaskini na kuinua kipato chao cha kila siku.
Amesema licha ya ajira kuongezeka kupitia viwanda hivyo pia itachangia ongezeko la kodi kwa serikali na kupelekea kuchangia pato la mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla na kueleza lazima wananchi wafahamu kuwa mafanikio yoyote hayapatikani bila kuwepo kwa viwanda.
Katika mradi huo zaidi ya makampuni 20 yamejitokeza kujenga viwanda eneo hilo ambapo ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwezi desemba mwaka huu.
Mwisho.

EmoticonEmoticon