Na Hamisi Ramadhani,Handeni.
MKULIMA
mmoja wa kijiji cha Sua Wilayani Handeni Mkoani Tanga, anashikiliwa na
Polisi Wilayani hapa kwa tuhuma za kukutwa na Bunduki mbili aina ya
magobole alizokuwa akizimiliki kinyume na sheria.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, alisema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 11.30 jioni katika kijiji hicho baada
ya raia wema kutoa
taarifa polisi.
Alisema
kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni baada ya wananchi kuwa na hofu na
ndipo raia wema wakatoa taarifa polisi kwa kuhofia kuwa mtuhumiwa huyo
anaweza kufanya uharifhu wakati wowote.
Alilitaja
jina la mtuhumiwa huyo kuwa ni Hamadi Ally Waziri (43) mkazi wa kijiji
cha Sua ambaye alikamatwa nyumbani kwake baada ya polisi kufanyiwa
upekuzi ndani kwake na ndipo wakazikuta bunduki mbili aina ya Magobole.
Kamanda
Massawe aliwapongeza raia wema kwa kutoa taarifa hizo na kuwataka kuwa
na ushirikiano na jeshi la polisi ili kuweza kutokomeza uhalifu ambayo
mkoani hapa.
Mwisho
EmoticonEmoticon