Na Oscar Assenga, Tanga.
TIMU ya Veteran leo imeanza vema mashindano ya ligi ndogo ya
Takukuru Cup baada ya kuilaza Makorora Star mabao 4-2 katika mchezo wa ufunguzi
wa michuano hiyo mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na timu
zote kuonekana kucheza kwa kukamiana ambapo mpaka timu zote zinakwenda
mapumziko timu ya Makorora Stars ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.
Mabao ya Makorora Star yakifungwa na Hussein Salim ambaye
alifunga mabao mawili kwenye dakika ya 6 na 45
Huku bao la Veteran FC la kwanza likipatikana kwenye dakika
ya 9 kupitia Sadiq Rashid ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao
hilo.
Kipindi chaa pili kilianza kwa kasi kwa kila timu kuingia
uwanjani hapo ikiwa na hari na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa
baadhi ya wachezaji wake ambapo, Veteran Sc walionekana kujipanga na kutaka
kulipa kisasi.
Wakicheza kwa kusikilizana Veteran Sc waliweza kuongeza bao
la pili ambalo lilifungwa na Tinath Tsungi katika dakika ya 55 huku Anderson
Solomoni akiipatia timu hiyo bao la pili ambalo lilipatikana kwenye dakika ya
58 kwa njia ya penati.
Baada ya kuingia mabao hayo,Veteran waliweza kuongeza kasi ya
mashambulizi langoni mwa Makorora na kufanikiwa kuandika bao lao la nne kupitia
Faridini Hemed dakika ya 84 ambalo lilihitimisha karamu ya mabao kwenye mchezo
huo.
Mashindano hayo yamefunguliwa leo na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Tanga ,Edson Makallo na yanashirikisha timu 4 ambazo ni Makorora Star,Magomeni Sc,Bomboka Sc na Veteran yenye lengo la kuhamasisha mapambano dhidi ya rushwa kupitia michezo mkoani Tanga.
Mwisho.
EmoticonEmoticon