Na Oscar Assenga, Tanga.
MASHINDANO ya Umoja wa shule
za Msingi nchini (Umitashumta) ngazi ya Mkoa wa Tanga yanatarajiwa kuanza
kutimua leo katika viwanja vitatu vilivyopo mkoani hapa.
Akizungumza na blog hii, Mratibu wa
Mashindano hayo, Rajabu Dimoso alisema maandalizi ya mashindano hayo
yanaendelea vizuri na yatashirikisha wanamichezo kutoka shule za wilaya tisa
zilizopo mkoani hapa na baadae kupatikana timu ambayo itashiriki ngazi ya Taifa.
Dimoso alizitaja wilaya hizo
kuwa ni Kilindi,Handeni,Pangani, Lushoto,Korogwe mjini na Korogwe vijijini,Muheza,Mkinga
na Tanga na kueleza mashindano hayo msimu huu yanatarajiwa kuwa ya aina yake
kutokana na ushindani uliokuwepo kwa timu hizo ngazi ya wilaya zao.
Aidha aliitaja michezo
itakayokuwa ikichezwa kwenye mashindano hayo kuwa ni mpira wa miguu,Pete, mpira
wa mikono ,wavu na riadha ambapo washindi watakabidhiwa zawadi zao baada ya
kumalizika michezo hiyo.
Alivitaja viwanja ambavyo
michezo hiyo itachezwa kuwa ni Mkwakwani, Popatlaly Sekondari na Shule ya
Sekondari Tanga Ufundi (Tanga School) ambapo michuano hiyo itashirikisha
wanamichezo wapatao 1098 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Afisa elimu Taaluma
Mkoa wa Tanga.
Mwisho.
“Bosnia kuzichapa na Ally
Baba”
Na Oscar Assenga, Tanga.
BONDIA Chipukizi Ally Bosnia wa
Tanga anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Ally Baba wa Kilimanjaro katika
pambano la nane lenye uzito wa kg71 lisilokuwa na ubingwa litakalifanyika Julai
7 mwaka huu kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.
Akizungumza jana, Muandaaji
wa Pambano hilo, Promota Abbasi Mwazoa alisema maandalizi ya pambano hilo
yanaendelea vizuri na kueleza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mabondia ambao
watacheza michezo kadhaa ya utangulizi.
Mwanzoa aliwataja mabondia
hao kuwa ni Khamisi Mwakinyo atachuana na Said Mundi katika pambano la raundi
nane lenye uzito wa kg61 ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake kabla ya Haji
Juma kupanda ulingoni kuzichapa na J.J.Ngotiko kwenye pambano litakalo kuwa la
kg 55 raundi sita.
Promota Mwanzoa aliyataja
mapambano mengine kuwa ni Athumani Boxers atakuwa na kibarua kizito dhidi ya
mpinzani wake Saimoni Zabron litakalouwa na raundi sita lenye uzito wa kg 61
huku Rajabu Mahoja nae akipanda jukwaani kuzichapa na Jumanne Mohamed pambano
la raundi sita lenye uzito wa kg 59.
Pambano lengine
litakalofanyika siku hiyo kuwa ni bondia Zuberi Kitandula atazichapa na Hemed
Kangeta litakalo kuwa la raundi 4 lenye uzito wa kg 55 wakati Abdalla Mapoka
naye atapambana na Ibrahimu Habibu pambano lenye uzito na raundi sawa na
mabondia hao.
Mwanzoa aliwataka
wadau wa mchezo masumbwi mkoani Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia mapambano
hayo ambayo yatakuwa na upinzani mkubwa kutokana na uwezo walionao mabondia
hao.
Mwisho.
EmoticonEmoticon