WATUMISHI wa serikali kutoka
idara mbalimbali mkoani hapa kesho jumamosi watachuana katika michezo
mbalimbali ikiwamo ya soka na netiboli katika bonanza litakalofanyika
uwanja wa shule ya Sekondari ya Tanga Ufundi.
Mkufunzi wa michezo mkoa
wa Tanga,Daniel Mabena alisema jana kuwa bonanza hilo litaratibiwa na Afisa
Michezo mkoani hapa, Digna Tesha na kufanyika asubuhi ambapo pia wadau
wengine wa michezo wanaruhusiwa kushiriki.
Alisema michezo
itakayochezwa katika bonanza hilo kuwa ni riadha,mazoezi ya viungo,kuvuta
kamba,netiboli,soka ambapo watacheza wanawake na wanaume.
Mkufunzi
huyo pia alisema katika bonanza hilo kutakuwa na semina fupi juu ya umuhimu
wa michezo kwa afya ambayo mafunzo yatatolewa na wataalamu kutoka idara ya
afya mkoa wa Tanga.
EmoticonEmoticon