KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOIPIGA NDANDA SC MABAO 2-1 UWANJA WA CCM MKWAKWANI. |
Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ambap ulikuwa na kasi kutokana na timu zote ksuhambuliana kwa zamu.
Mabao ya Coastal yalifungwa na Joseph Mahundi akimaliza pasi ya Hamisi Mbwana "Kibacha" na bao la pili likifungwa na Hussein Sued aliyemaliza krosi ya Razack Khafani.
Bao la kufutia machozi la Ndanda FC lilifungwa dakika ya 57 kupitia Nassoro Kapamba kwa njia ya penati iliyotokana na mchezaji wa Coastal Union Sabri Rashid kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Amoni Paul kutoka Mara kuamuru ipigwe penati hiyo.
EmoticonEmoticon