-Fursa lukuki za kiuchumi zaibuliwa
DP WAIBUKA NA SERA YA KUBORESHA KANUNI ZA KIKOKOTOO ENDAPO WATAPATA RIDHAA YA KUONGOZA NCHI
siasaMluya ambaye aliambatana na mgombea mwenza Saodun Abraham Khatibu ameyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliopo jijini Dodoma.
Amesema suala la Kikokotoo kwa watumishi imekuwa changamoto kubwa sana kwa watumishi hivyo DP inakwenda kulifanyia kazi suala hilo ili watumishi waweze kupata mafao yao bila changamoto yeyote
"Tunakwenda kufuta kilio cha Kikokotoo kwa watumishi,haiwezekani mtu afanye kazi ndani ya miaka 33 halafu alipwe mafao sh milioni 13 hadi 14 hilo tunakwenda kuliondoa,"amesema Mluya.
Amesema serikali ya DP itakwenda kuwajengea nyumba watumishi ambao wamekaa ofisini zaidi ya mwaka bila kashfa ya kosa lolote lile ili kusaidia kuondoa rushwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mbali na hayo pia amesema DP itashughulikia na kuboresha maslahi ya Jeshi la Magereza pamoja na majeshi mengine ili kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira bora na kuongeza kuwa wataboresha pia suala zima la Magereza ya wafungwa hapa nchini.
Mluya amesema vipaumbele vingine kwao ni suala la Afya,ambapo kinamama watajifungua bure na mtoto atapewa lishe kwa miezi mitatu huku akisema marehemu hatadaiwa hela ya matibabu,ndugu watapewa mwili ili wakazike na kwenye kilimo watahimiza kilimo cha umwagiliaji.
KYARA WA SAU ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI INEC KUWANIA KITI CHA RAIS UCHAGUZI MKUU 2025
Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe.
Majalio Paul Kyara na Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) wakionesha mkoba wa fomu za uteuzi waliokabidhiwa na Tume leo Agosti 13, 2025. (Picha na INEC).
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs
Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa
Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU) Mhe. Majalio Paul Kyara. Mgombea huyo
waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Satia Mussa Bebwa (kushoto) alichukua
fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27
mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan
Kailima. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu
za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe.
Majalio Paul Kyara. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Satia
Mussa Bebwa (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume
inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima akimwelekeza mgombea Mhe. Majalio Paul Kyara namna ya kujaza kusaini kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe. Majalio Paul Kyara akisaini kitabu
Mgombea Mwenza, Mhe. Satia Mussa Bebwa akisaini kitabu huku akishuhudiwa na Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe. Majalio Paul Kyara.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.
Mgombea Mwenza, Mhe. Satia Mussa Bebwa akisaini kitabu huku akishuhudiwa na Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Mhe. Majalio Paul Kyara.
Wanahabari wakiwa katika ukumbi wa kutolea fomu wakichukua matukio.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza.
Wanachama wa SAU wakiwa ukumbini hapo.
Wanachama wa SAU wakiwa ukumbini hapo.
Wagombea wakiwa ukumbini.
SERIKALI ITAENDELEA KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA: MHE. UMMY NDERIANANGA
habariNa; Mwandishi Wetu – Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuweka mazingira wezeshi ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Mhe. Ummy Nderiananga amesema hayo wakati wa akihitimisha maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa tarehe 12 Agosti, 2025 katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.
Amesema kuwa, vijana ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana naoi li kuwekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa.
“Tanzania ina idadi kubwa ya vijana na kati yao wenye umri wa miaka 15 hadi 35 ni asilimia 34.5, kwa kutambua umuhimu wa vijana kama nguvu kazi ya Taifa Serikali ipo tayari kuhakikisha vijana wanawezeshwa ili waweze kufikia malengo yao,” amesema
Aidha, Naibu Waziri Nderiananga amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu programu za vijana zinazotekelezwa na Wizara nyingine katika sekta mbalimbali nchini. Pia, programu za uwezeshaji vijana kiuchumi kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana, mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri na mifuko mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi lengo ikiwa kuwezesha vijana kunufaika na mikopo himilivu itakayowasaidia kuanzisha miradi itakayowawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wenzao.
Vile vile, amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu programu ya Taifa ya kukuza Ujuzi kwa vijana ambapo vijana hupatiwa mafunzo ya ufundi stadi, ujasiriamali na stadi za kazi kupitia vyuo vya ufundi stadi vilivyopo nchini. Ameongeza kuwa, Serikali imepanga kuanzisha ‘Skills Development Center for Overseas Employement’ ili kuwasiaida vijana wa kitanzania wanaotafuta fursa za ajira nje ya nchi wanaunganishwa na fursa hizo na wanaweza kumudu ushindani wa soko la ajira.
Kwa upande mwengine, Mhe. Ummy Nderiananga amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo ili kukuza ustawi wao na kuhakikisha malengo ya vijana yanafikiwa.
Naye, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Dkt. Majaliwa Marwa amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali Pamoja na asasi zinazo ongozwa na vijana kukuza ujuzi na kidijitali kupitia vituo vya ubunifu, kuwezesha ushiriki katika ujenzi wa amani, uongozi na majadiliano ya kijamii, kuongeza huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana na kuimarisha mifumo ya takwimu, ujumuishi na uwajibikaji ili kuhakikisha hakuna kijana anasahaulika.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Vijana Bw. Arafat Lesheve ameiomba serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na jamii kwa ujumla kuendelea kuwezesha, kusikiliza na kushirikisha vijana katika kila hatua ya maendeleo ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.










SERIKALI YALIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 999 KWA WANANCHI 103 WA DODOMA KWA MIRADI YA MAJI
habariAfisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Ambrosi Siril akimsaidia mzee Peter Mazengo kusaini katika daftari la fidia katika eneo la Zuzu Nala jijini Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa na DUWASA. Agosti 11,2025
DODOMA, Agosti 12, 2025
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Maji, imekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia yenye jumla ya Shilingi Milioni 999 kwa wananchi 103 ambao ardhi yao ilitwaliwa katika maeneo ya Nzuguni, Zuzu Nala, Nala Chihoni na Kibaigwa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).
Ulipaji wa fidia hizo, umeongozwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA, Wizara ya Ardhi na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa maeneo husika, ambapo kwa eneo la Nzuguni, Wananchi 24 wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 148 tarehe 07 Agosti, 2025,.
Aliyekuwa Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akipokea hundi kutoka kwa Muhasibu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Getrude Mosha wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa Zuzu Nala jijini Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa na
DUWASA. Agosti 11,2025
Alitaja wengine kuwa ni Zuzu Nala Wananchi 51 ambao wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 594 Agosti 11, 2025, Nala Chihoni Wananchi 7 ambao walilipwa fidia yao ya Shilingi Milioni 58 tangu mwezi Aprili, 2025 na Kanda ya Kibaigwa Wananchi 23 wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 197 na kukamilisha zoezi hilo Agosti 12, 2025.
Muhasibu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Getrude Mosha (kulia) akizungumza na mkazi wa Nzuguni wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa Nzuguni jijini Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa na DUWASA. Agosti 11,2025
Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa wananchi waliyotoa ardhi yao kupisha utekelezaji wa miradi ya maji.
Mkazi wa Nzuguni, Benjamini Elias akisaini katika daftari la fidia wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa Nzuguni jijini Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa na DUWASA. Agosti 11,2025
"DUWASA, kwa niaba ya Wananchi wa maeneo ya Nzuguni, Zuzu Nala, Nala Chihoni na Kibaigwa, inaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita na Wizara ya Maji kwa juhudi zao kubwa na ufanisi katika kuhakikisha ulipaji wa fidia kwa wakati kwa wananchi wetu," alisema Mhandisi Aron.
"Hatua hii ni muhimu sana kwa maeneo yaliyotekelezwa na yanayoendelea na utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati katika Jiji la Dodoma na Kanda ya Kibaigwa, hii inaonesha dhamira ya Serikali katika kulinda haki za wananchi wakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo." Amesma Mhandisi Aron.
Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Maji, Moses Mgalla, akizungumza na wananchi wa Kibaigwa ambao maeneo yao yamechukuliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa Mji wa Kibaigwa jijini Dodoma. Agosti 12,2025
Kwa upande wa wakazi wa Kibaigwa, Bi. Josephina Paulo ameishukuru serikali kwa kuwasikiliza na kuwalipa fidia. Ameiomba serikali kwa kuwaona wanyonge na kuwafikia wengine ambao bado hawajalipwa wanasubiri kulipwa.
Naye Bwa. Yohana Mwarabu ameshukuru serikali kwa kumjali na kumlipa kwani sasa ataenda kujenga nyumba nyingine ili aweze kuishi na familia yake kwani awali hakuwa na matumaini lakini kwa sasa anaamani.
Fidia hiyo ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia DUWASA iliyokusudiwa kuboresha upatikanaji wa majisafi na huduma za usafi wa mazingira ka wakazi wa jiji la Dodoma na maeneo mengine yanayohudumiwa na DUWASA.
Subscribe to:
Posts (Atom)