MLUYA WA CHAMA CHA DP ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI INEC KUWANIA KITI CHA RAIS

August 13, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP), Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 13, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima, akimwelekeza Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.

Mgombea Mwenza, Mhe. Sadoun Abrahman Khatib akisaini kitabu huku akishuhudiwa na Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akisaini kitabu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto aliyeketi ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima.



Wanachama wa Chama cha Democratic Party wakiwa katika ukumbi wa kutolea fomu wakifuatilia matukio.

Wanachama wa Chama cha Democratic Party wakiwa katika ukumbi wa kutolea fomu wakifuatilia matukio.

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, 
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Mhe. Abdul Juma Mluya akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu.




MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. SAMIA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA FEDHA ZA KAMPENI

August 13, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi, wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CCM na Watanzania wapenda maendeleo katika harambee ya kuchangisha fedha, iliyolenga kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya kampeni za CCM za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025,hafla hiyo inaendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam.









KIMARO ACHANGIA MILIONI 20 HARAMBEE YA CCM

August 13, 2025 Add Comment

 


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara  maarufu jijini Arusha,Ndugu Nathan Kimaro ametoa kiasi cha shilingi milioni 20 kama sehemu ya mchango  wake wa kusaidia kampeni za uchaguzi wa wagombea wa Urais wa chama hicho Oktoba,2025.


Kimaro mbali ya kuchangia lakini pia alikuwepo ukumbini hapo jana Agosti 12,2025, kushuhudia ‘LIVE’ hafla hiyo ya Harambee ikiendelea ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Harambee hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,ikilenga kukusanya kiasi cha fedha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.


Aidha katika harambee hiyo,Chama cha Mapinduzi (CCM) kilifanikiwa kuchangisha kiasi cha fedha, jumla ya shilingi Bilioni 86.31 zikiwemo na ahadi,ambapo kuchangia huko kutafika tamati Agosti 27,2025 .

ZANZIBAR YACHOTA UZOEFU DODOMA,YAJIANDAA KUJENGA MJI WA SERIKALI KISAKASAKA

August 12, 2025 Add Comment

 



Kamati ya wataalamu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikiingozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum imetembelea miradi mikubwa jijini Dodoma ikiwemo Mji wa Serikali Mtumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, kujifunza utekelezaji wa Ujenzi wa Mji wa Serikali.

Ziara hiyo inalenga kuandaa mazingira ya ujenzi wa ofisi za Serikali na Baraza la Wawakilishi eneo la Kisakasaka, Zanzibar.

Viongozi hao wamempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuimarisha maendeleo ya Makao Makuu ya Nchi kupitia miradi ya kimkakati. 

#Dodoma #Zanzibar #MjiWaSerikali #Tanzania




DKT.EGBERT MKOKO - BLOG ZISITUMIKE VIBAYA UCHAGUZI MKUU

August 12, 2025 Add Comment


 Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM –

 Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), Dkt. Egbert Mkoko, amewataka waendeshaji wa blogu nchini kuepuka kuzitumia vibaya katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 

 Akizungumza katika mafunzo maalumu ya bloga yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ombi la Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN), Dkt. Mkoko alisema blogu zina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii, hivyo zinapaswa kutumika kwa uangalifu na weledi. 


 “Blog zina nguvu kubwa ya kusambaza taarifa kwa jamii, hivyo mnapaswa kuzitumia vizuri hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaingia kwenye uchaguzi mkuu,” alisema. 

 Alibainisha kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Mwongozo wa Uandishi wa Habari za Uchaguzi ili kuhakikisha taarifa zinazochapishwa zinachangia kudumisha amani na utulivu nchini. 

 Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, aliwakumbusha wanahabari kuepuka kuandika taarifa za uzushi na uchochezi ambazo zinaweza kusababisha taharuki. 

Alisisitiza umuhimu wa kutoa nafasi sawa kwa vyama vyote vya siasa na kuthibitisha ukweli wa taarifa kwa mamlaka husika kabla ya kuziweka hadharani.


 Naye Dkt. Darius Mukiza wa SJMC, akitoa mada kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Akili Bandia (AI) kuelekea uchaguzi mkuu, alisema teknolojia hiyo haitaepukika katika nyanja za mawasiliano.

 

Alifafanua kuwa AI inarahisisha kazi, inafanya kazi kwa kasi, gharama zake ni nafuu, na inaweza kutafsiri lugha nyingi kwa wakati mmoja, lakini pia ina changamoto zake endapo itatumika vibaya.


 “Akili Bandia ikitumika vizuri inaongeza ufanisi wa mawasiliano, lakini ikitumiwa vibaya inaweza kuwa na madhara makubwa. Ni jukumu la watumiaji kuzingatia maadili na weledi,” alisisitiza.





. Mafunzo hayo yamekusudia kuwajengea uwezo waendeshaji wa blogu kuhusu uandishi wa habari za uchaguzi, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na teknolojia mpya ili kuchangia uchaguzi wenye amani na maadili.