SHUKRANI KWA KUTEKELEZA AHADI YA NYONGEZA YA MSHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA

August 12, 2025 Add Comment

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamhokya, na ujumbe wake Pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025.

Picha Namba 01: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Agosti, 2025. Viongozi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji wa ahadi yake ya nyongeza ya mishahara, kupanda madaraja ya watumishi wa umma na kuboresha mazingira ya kazi nchini.







WATANZANIA TUSIKUBALI UCHAGUZI UTUGAWE - DKT. BITEKO

August 12, 2025 Add Comment

 WATANZANIA TUSIKUBALI UCHAGUZI UTUGAWE - DKT. BITEKO



📌 Asema Kuna Maisha baada ya Uchaguzi


 ðŸ“Œ Amwakilisha Rais Samia,miaka 40 Kanisa Anglikana Dayosisi ya Kagera


📌 Rais Samia achangia Tsh. Milioni 50 Ujenzi wa Kanisa Dayosisi ya Kagera


📌 Anglikana Waishukuru Serikali, washirika wa maendeleo


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuwapima wagombea wa nafasi mbalimbali  katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuchagua kwa haki ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025 (mwaka huu) na katu wasikubali Uchaguzi uwagawe.


Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji - Murgwanza, Ngara.

Amesema kuwa watanzania wanayo haki ya kuwapima wagombea kwa matendo yao na hatimaye kutenda haki kwa kufanya uchaguzi wao kwa njia ya demokrasia huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia kampeni za kistaarabu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa maadili.

Akiwasilisha salamu za Mheshimiwa Rais, Dkt. Biteko amesema Dkt. Samia anatambua na kuheshimu mchango wa taasisi za dini na mchango wake katika maendeleo ya Taifa. “ Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mdau wa kujenga na kila mnachokifanya kinalenga katika maendeleo ya watu hivyo anaunga mkono jitihada za maendeleo ya wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Katika kufanikisha azma yake, Rais Dkt. Samia amechangia shilingi milioni hamsini (50,000,000/=) katika harambee ya ujenzi wa Kanisa jipya la Anglikana Dayosisi ya Kagera.


Dkt. Biteko Amesisitiza umuhimu wa kila mtu kuwa kisababishi cha furaha kwa mwenzake ili kuwa na maisha ya ya furaha.

Awali, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Kagera, Darlington Misango Bendankeha ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa unaopatikana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Askofu Bendankeha amesisitiza kuwa Serikali katika ngazi zote inatoa ushirikiano na hivyo kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Afya, Elimu kwa maendeleo ya jamii.

Ameiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Barabara inayounganisha taasisi mbalimbali za utoaji wa huduma yenye urefu wa mita 900, Gari la wagonjwa pamoja na mchango wa ujenzi Kanisa ambalo ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.18


Kufuatia maombi hayo, Dkt. Biteko amemwelekeza Mkuu wa Mkoa, Mkuu Wilaya na Wakala wa Barabara mijini na vijijini (TARURA) kufanikisha ujenzi wa Kipande hicho huku akitoa ahadi ya gari la wagonjwa katika Hospitali ya Murgwanza baada ya kuwasiliana na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama.

Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao, Askofu Bendankeha amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu na kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi Mkuu ujao ili kuchochea maendeleo “ Tujiandae kushiriki uchaguzi Mkuu ujao, kura yetu ndiyo nguvu ya mabadiliko.” Amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatuma Mwassa amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa huduma mbalimbali za maenseleo zinazotolewa kwa jamii.




MWISHO

CHAUMA WACHUKUA FOMU ZA UTEUZI INEC

August 12, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Devotha Mathew Minja (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Devotha Mathew Minja (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.  (Picha na INEC).



MGOMBEA CCK ACHUKUA FOMU ZA UTEUZI

August 12, 2025 Add Comment

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii  (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii  (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.  (Picha na INEC).


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii  (CCK), Mhe. David Daud Mwaijojele. Mgombea huyo waaliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe.  Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima.  (Picha na INEC).


KAYA 3,255 KUNUFAIKA NA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU WILAYA YA MLELE

August 12, 2025 Add Comment
-Wananchi waipongeza Serikali kwa makati huo