Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa (kulia) na Rais wa Botswana Mhe. Duma Boko kabla ya kuanza Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

![]() |

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe.James G. Bwana katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP)
Na Mwandishi Maalumu
RAIS Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki
katika Mkutano Mkuu wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika (AU-AIP
Water Investment Summit) unaoendelea jijini Cape Town, Afrika Kusini.
Dkt. Kikwete amehudhuria mkutano huo kwa nafasi yake ya
Mwenyekiti Mwenza Msaidizi (Alternate Co-Chair) wa Jopo la Ngazi ya Juu la
Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (The High Level Panel on the Africa Water
Investment Programme – AIP).
Mwaka huu, Afrika Kusini ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 20
(G20). Viongozi wa Afrika wanaokutana Cape Town wanataka Programu ya Uwekezaji
wa Maji Afrika iwe miongoni mwa ajenda kuu katika Mkutano ujao wa G20,
uliopangwa kufanyika Novemba 2025 jijini Cape Town.
Mkutano huu umeitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa
kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini na Jopo la Ngazi ya Juu la AIP.
Jopo hilo linaongozwa na Wenyeviti Wenza Watatu – Rais wa
Namibia, Rais wa Senegal, na Waziri Mkuu wa Uholanzi. Wajumbe wengine ni Marais
wa Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Gambia, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), pamoja na Mfalme wa Morocco. Dkt. Kikwete, akiwa Mwenyekiti Mwenza Msaidizi,
anasaidia Wenyeviti Wenza katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mkutano ulifunguliwa na Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Rais wa
Afrika Kusini na Mwenyekiti wa G20 kwa mwaka 2025. Washiriki wengine wakuu ni
pamoja na Mfalme Mswati wa III wa Eswatini, Mhe. Duma Boko – Rais wa Botswana,
pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali, mashirika, na wadau wa maji kutoka
kote barani Afrika.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kikwete ameteuliwa kuwa mmoja wa
viongozi wakuu watano wa Baraza la Uwezeshaji wa Uenyekiti wa Afrika Kusini wa
G20 mwaka huu 2025, akishughulikia masuala ya maji kama Mwenyekiti Mwenza
Msaidizi.
Wengine ni Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan wa Umoja wa
Falme za Kiarabu (Co-Chair), Waziri Mkuu Mia Mottley wa Barbados (Co-Chair),
Bw. Bill Gates – Mwenyekiti wa Mfuko wa Gates (Co-Chair), na Mheshimiwa Amina
J. Mohammed – Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Alternate Co-Chair).
EmoticonEmoticon