RAIS SAMIA AWAFUTA MACHOZI YA KUNI AKINA MA NCHINI

August 05, 2025 Add Comment


*📌Atoa Ruzuku ya shilingi bilioni 9.4 kwenye Majiko Banifu*


*📌Kaya 200,000 kunufaika*


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa shilingi 9,400,799,626.7  wa kusambaza majiko yaliyoboreshwa maarufu kama majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku ya asilimia 80 hadi 85 kote nchini.


Hayo yamesemwa Agosti 4, 2025 na mwakilishi wa REA Mkoani Morogoro, Mhandisi Cecilia Msangi wakati akimtambulisha Mtoa huduma aliyeshinda zabuni ya kusambaza majiko hayo Mkoani humo, kampuni ya Burn Manufacturing Tanzania Ltd katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

"Wakala unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia miradi mbalimbali ikiwemo huu wa kusambaza majiko banifu ambao rasmi leo hii tupo hapa kuutambulisha kwa wananchi wa Morogoro," alisema Mha. Msangi.


Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kampeni hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia ambayo alisema kwa jitihada zake binafsi hatua mbalimbali zimechukuliwa  hususan za kuwanusuru akina mama kutokana na madhara ya moshi wa kuni sambamba na uhifadhi wa mazingira.

Alisema Rais Samia alitoa maelekezo mahususi ya kuhakikisha wananchi wanawezeshwa ili kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kupikia ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umeelekeza ifikapo Mwaka 2034; 80% ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.


Akizungumza juu ya utekelezaji wa mradi kwa Mkoa wa Morogoro, Mha. Msangi alisema jumla ya majiko banifu 8,366 yatatolewa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 14,694 kwa kila jiko.


"Kwa bei ya kawaida kabla ruzuku jiko hilo lilikuwa likiuzwa shilingi 73,468.36 na sasa baada ya kupokea kwa ruzuku ya 80% jiko hilo litauzwa kwa shilingi 14,694 tu," alibainisha Mhandisi Msangi.


Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Mussa Mussa alipongeza jitihada za REA na alisema kuwa manufaa yatakayopatikana kutokana na mradi huo ni makubwa kuliko hata inavyotarajiwa.


"Haya majiko namna yalivyosanifiwa yanatumia mkaa kidogo na pia yanatunza joto kwa muda mrefu, hivyo inakwenda kumpunguzia mwananchi gharama za mkaa na kumuokolea muda," alisisitiza Katibu Tawala, Musa.


Aidha, mwakilishi wa Mtoa huduma Kampuni ya Burn Mkoani humo, John Mtui alisema kampuni yao imeshinda zabuni ya kusambaza majiko banifu 39,286 katika Mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Kagera na Tabora ambayo ni sawa na shilingi 2,309,022,392.77.


"Hapa Morogoro tutasambaza jumla ya majiko 8,366 katika Wilaya za Gairo, Kilombero, Kilosa, Malinyi, Morogoro Vijijini, Ulanga na Mvomero ambapo kila wilaya itapata majiko 1,196," alisema Mtui.


REA inatekeleza miradi mbalimbali nchini kwa kuwezesha na kuelimisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati zisizo safi na salama kwa afya zao na mazingira kwa ujumla.

UMMY MWALIMU ASHINDA KURA ZA MAONI JIMBO LA TANGA MJINI

August 05, 2025 Add Comment



Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tanga Mjini wamemchagua ndugu. Ummy Ali Mwalimu kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo kwa kura 5,750 kati ya kura 10,293 zilizopigwa.


Akitangaza matokeo hayo August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Tanga Mjini linajumla ya wajumbe 12,620 na waliopiga kura ni 10,293 ambapo kura zilizoharibika ni 117, kura halali zilizopigwa ni 10,176 sawa na Wastani wa asilimia 56.5


Ummy Ali Mwalimu amepata kura 5,750 ambayo ni sawa na 56.5%, Omary Ayoub akipata 4,146 sawa na 40%, Kassim Mbaraka 80 sawa na 1%, Rajabu Abasi 130 sawa na 1% huku Arif Fazel akipata kura 70 sawa na 0%.

RAIS SAMIA AWAFUTA MACHOZI YA KUNI AKINA MAMA NCHINI

August 05, 2025 Add Comment
-Atoa Ruzuku ya shilingi bilioni 9.4 kwenye Majiko Banifu

ENG JOHNSTON MTASINGWA AWAGARAGAZA 4 KURA ZA MAONI BUKOBA MJINI

August 04, 2025 Add Comment



Na Mariam Kaagenda_Kagera 


Mhandisi wa TANROAD, Johnston Mtasingwa ameibuka mshindi katika Uchaguzi wa  Kura za maoni Jimbo la Bukoba Mjini  kwa kupata kura 1,408 na kuwabwaga wenzake  wanne waliokuwa wakishiriki mchakato wa kumpata Mbunge kupitia  Chama Cha Mapinduzi (CCM) 


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Bukoba Mjini, Shabani Mdohe ametangaza  matokeo ya kura za maoni ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis ambaye amepata Kura  804 , Almasoud Kalumuna kura 640 Jamila Hassan kura 66 na Koku Rutha kura 44


 Wapiga kura waliojiandikisha ni 3033 waliojitokeza kupiga kura ni 2978 ambapo Kura  zilizoharibika ni kura 20 na kura halali ni 2958.

BUKOMBE WAMCHAGUA DKT.BITEKO KWA ASILIMIA 99.8

August 04, 2025 Add Comment



Wajumbe wa Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe wamemchagua Dkt. Doto Mashaka Biteko kwa asilimia 99.8 baada ya kupata kura 7,441 kati ya kura 7,456 zilizopigwa ili apeperushe bendera ya Chama hicho.


Akitangaza matokeo hayo August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Bukombe linajumla ya wajumbe 7,835 na waliopiga kura ni 7,456 ambapo kura zilizoharibika ni 15, kura za hapana ni 0, kura halali zilizopigwa ni 7,441.


Kwa matokeo hayo, Dkt. Doto Mashaka Biteko amepata kura 7,441 kati ya 7,456 sawa na wastani wa asilimia 99.8 uchaguzi uliofanyika katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.


Mwisho.