UWEKEZAJI WA SERIKALI KATIKA BANDARI YA TANGA WAENDELEA KULIPA TPA NA TRA ZAKUSANYA BILIONI 484.8 KWA MIEZI 24.

July 12, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga Tanga


FEDHA zilizotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 kwa ajili ya uwekezaji katika bandari ya Tanga, fedha hizo zimerudi na kubaki salio la shilingi bilioni 56.7.

Hayo yalisemwa na  Meneja wa bandari ya Tanga Mhandisi Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa kwa kipindi cha miezi 24 taasisi mbili za serikali za TPA na Mamlaka ya mapato nchini TRA, wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 484.8.

Alisema kutokana na makusanyo hayo ile fedha iliyotolewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 429.1 imesharudishwa na taasisi mbili za TPA na TRA kwa miezi 24 na chenji pembeni imebaki na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huo.

Akifafanua kuhusu makusanyo hayo alisema kwamba TPA  imeendelea kuvunja rekodi ya mapato kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali na kupelekea ongezeko la shilingi bilioni 30 ya mapato ambayo waliwekewa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 45.56 hadi kufikia makusanyo ya shilingi bilioni 75.139.

Aidha alisema katika mwaka wa 2023/2024 Bandari ya Tanga iliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 38.7 tofauti na makusanyo ya shilingi  bilioni 75.139 ikiwa ni ongezeko la asilimia 94.

Meneja huyo alisema makusanyo hayo ni kwa taasisi mbili za serikali ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka wa fedha 2024/2025 waliweza kukusanya shilingi bilioni 215 kati ya hizo Bilioni 107 zimetoka Bandari ya Tanga kupitia mizigo mchanganyiko.

Pia alisema kwa upande wa makusanyo ya mafuta waliweza kukusanyia kiasi cha shilingi  bilioni 108 hivyo ukichukua makusanyo hayo kwa taasisi hizo ni kiasi cha shilingi bilioni 215.22  na TPA wamekusanya shilingi bilioni 75.159 na kufanya jumla kuwa shilingi bilioni 290 ambazo zimeweza kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kipindi cha miezi  24.

Aliongeza  kutoka mwaka 2023/2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA) waliweza kukusanya kiasi cha Bilioni 195 na ni taasisi mbili tu kwa mchanganuo huo kwamba TPA walikusanya Bilioni 38.7 na TRA walikusanya Bilioni 156.75  hiyo jumla yake ni zaidi Bilioni 195.

Alieleza kwamba ukichukua miezi 24 mwaka 2023/2024 ilikuwa ni Bilioni 195 na pointi zake  na 2024/2025 nilikuwa ni bilioni 290 ukizijumulisha zote unapata kwa miezi 24 TRA na Bandari ya Tanga imeweza kukusanya Bilioni 485.8. 

Meneja huyo alisema kwamba katika Bandari ya Tanga  June 30 mwaka huu, mwaka wa fedha uliomalizika wameweza kuhudumia shehena tani milioni 1,416,127  wao wamefanikiwa kuhudumia mertiki tani milioni 1,326,415.

Alieleza katika mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 bandari iliweza kuhudumia metric tani milioni 1,191,480 ukichukua tofauti ya mwaka huu na mwaka 2023/2024 na mwaka 2024/2025 waliohudumia watapata tofauti ya laki 1,340,000 utaona kuna ongezeko la asilimia 11.3 kati ya mwaka 2023/2024 na mwaka 2024/2025 bandari imeweza kuongeza kiwango cha kuhudumia shehena.
Akizungumzia kuhusu meli zilizohudumiwa na Bandari hiyo alisema kwamba walipewa lengo la kuhudumia meli 222 lakini kwa mwaka wa fedha 2024/2025  baada ya kupewa malengo hayo wameweza kuhudumia meli 458 katika meli hizo meli 148 za Bahari kuu na Meli 310 ni za Mwambao.

Mwaka 2023/2024 Bandari ya Tanga iliweza kuhudumia meli 307 utaona kuna tofauti ya meli 151 ni sawa na asilimia 49.1 wameongeza idadi ya kuhudumia meli zaidi  na upande wa makasha walipewa lengo la kuhudumia makasha 8,351 lakini wamefanikiwa kwa mwaka wa fedha 9,026 ni ongezeko la asilimia 8 lakikni mwaka 2023/2024 waliweza kuhudumia makasha tools  7,817 ukiangalia ni ongezeko la asilimia 15.46 ,
Upande wa abiria mwaka 2024/2025 walipewa lengo la kuhudumia abiria 120,000 lakini hawakufanya vizuri waliweza kuhudumia kwa asilimia 50 ambapo abiria 59,960 waliweza kuhudumiwa kwa kipindi cha mwaka 2024/2025.

Alisema mwaka wa nyuma yake 2023/2024 waliweza kuhudumia abiria 62,904 hiyo kwa sababu katika eneo hilo ni wadau binafsi wenye meli ndio wenye jukumu la wa kuwasafirisha abiria kutoka Tanga kwenda maeneo mengine kama Zanzibar maeneo ya Pemba na Unguja

Mwisho.

PINDA ATAKA HAKI MCHAKATO WA WAGOMBEA

July 11, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga,TANGA

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mizengo Pinda amehimiza viongozi waliopewa dhamana ya mamlaka ya kusimamia mchakato wa uteuzi wa wagombea kuhakikisha wanatenda haki kwa wale wote waliojitokeza kwenye kinyang’anyiro hicho .

Pinda aliyasema hayo leo mara baada ya kutembelea ukarabati wa ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga ambao umefikia asilimia 99 uliofanywa ikiwa ni ndoto za Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Rajab Abduhaman kuona jengo hilo linakuwa na muonekana mzuri kwa ajili ya kuwahudumia wana CCM.

Akiwa katika eneo hilo mara baada ya kutembelea ukarabati wa jingo hilo aliupongeza uongozi wa CCM kutokana na kazi nzuri walioifanya ya kukarabati jengo hilo na hivyo kuwa na muonekana mpya.

Alisema wakati nchi ikielekea kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu tayari maandalizi yameshaanza na waliochukua fomu Udiwani na Ubunge wameshafanya na kazi ya chama ni kuhimiza viongozi waliopewa dhamana ya mamlaka ya kusimamia mchakato watende haki.

“ Bahati nzuri kamati yenu mlisimamie kikamilifu ili mtu asipate sababu ya kupiga kelele wakati hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa wananchi tunaomba wakati wa kupiga kura tumieni haki yenu tena kwa uhuru wenu wenyewe”Alisema

Aidha alisema pia kupitia utaratibu uliowekwa kabla ya kutoka kwenda kupambana na vyama vyengine lazima wampate mgombea wa chama atakayekwenda kupambana na vyama vyengine vya siasa tumieni haki yenu vizuri mtupe mgombea ambaye mnaamini anaweza kutuvusha kwa haraka zaidi.

Hata hivyo Waziri Mkuu Mstaafu Pinda alisema kwamba wanaendelea kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu na kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya nchi ipo kwenye utulivu na amani na mambo yanasonga mbele.

“Tanga kuna maneno nimesikia Rais hana deni na sisi na octoba tunatiki niombeni wana Tanga na wana CCM hilo jambo lipo mbele yenu na Tanga mlikuwa wapambanaji sana lazima jitihada kuhakikisha mnaongoza kwenye kura za Rais na Ubunge kwenye chaguzi zijazo”Alisema

Pinda aliwataka viongozi wa mkoa huo kuendelea kuchapa kazi pamoja na mshikamano kwa kuhakikisha wanaendelea kudumisha amani na ulitulivu ambao wanao mpaka sasa kutokana na kwamba haukudondoka tu angani bali umejengwa hivyo waendelee kumuomba mwenyezi Mungu aendelee kuisimamia.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman amesema ukarabati wa ofisi hiyo ni maelekezo ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Dkt Samia Suluhu kuhakikisha mali za chama yakiwemo majengo ya chama ya ofisi na menginevyo wanayalinda na kuyafanyia ukarabati mkubwa ili yaendelee kutumika miaka mingi kadri inavyowezekana.

Aidha alisema kwamba alifanya ziara kwenye mkoa wa Tanga na katikati pita pita yake aliona jengo lao namna lilivyokuwa na kutoa maelekezo kuhakikisha jengo hilo linafanyiwa ukarabati mkubwa na hayo ni matunda ya Mwenyekiti wa Taifa na maelekeo yake.

“Tulipopata maelekezo hayo tukasema lazima tufanye kwa sababu haki na heshima ya CCM kwenye nchi na mkoa wa Tanga ni kubwa haiwezekani viongozi wa CCM wanaovyoonekana uzuri lakini mahali wanapofanyia kazi hapafanani na nasi tukasema hapana lazima watii maelekezo hayo na tunashukuru wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na Kamisaa wao kwa umoja na mshikamano wao ndio umewezesha kutekeleza maelekezo hayo ya Rais”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi ,Dkt Batilda Burian amesema wa wamefarijika uwepo wa Waziri Mkuu huyo na wanamshukru Mwenyekiti Taifa kwa kazi kubwa aliyoifanya wakati wa ziara yake na wana Tanga wanaendelea kumshukuru kwa mambo mengi makubwa ya kimaendeleo aliyofanya kwa mkoa huo.

“Kutokanana na hilo tunasema kwamba Mama Hana deni na Octoba tunatiki na kura zitajaa na kumwagika kutokana na kasi kubwa ya maendeleo aliyoyafanya katika mkoa wa Tanga na hivyo kuufungua kiuchumi”Alisema

Hata hivyo,Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Mfaume Kizigo alisema chama hicho kimepata kiongozi wa kwelikweli na kinachoonekana hapo ni sehemu ya maendeleo makubwa yaliyofanywa na Mwenyekiti huyo kutokana na kila wilaya amejenga byumba za watumishi kuanzia chama na Jumuiya zake zote na amefanya hivyo kila alipokwenda kuishauri kamati ya siasa.



Mwisho.





















KAMISHNA BADRU ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA NA KUPONGEZA JITIHADA ZA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI

July 11, 2025 Add Comment

 


Na Hamis Dambaya, DSM.

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Abdul-Razaq Badru ametembelea maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa  sabasaba na kupongeza kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya banda  hilo Kamishna Badru amezipongeza taasisi hizo kwa kushinda tuzo nyingi zilizotolewa na mtandao wa World Travel Awards (WTA) by 28 Juni, 2025

Kamishna Badru amewaeleza  waandishi wa habari kuwa sambamba na ushiriki wa Ngorongoro katika maonesho mbalimbali ili kujitangaza , pia mamlaka hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu ya utalii kama barabara, huduma za malipo, malazi kwa wageni na huduma za usafiri.

“Tumejipanga mwaka huu wa fedha kuhakikisha kuwa barabara zetu zinaboreshwa na kupitika muda wote, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jitihada zinaendelea kuongeza miundombinu ya malazi na huduma za usafiri ili kukidhi ongezeko la wageni wanaotembelea vivutio vyetu kila mwaka,”alisema Kamishna Badru.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inashiriki maonesho hayo ili kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kwa watembeleaji wa eneo hilo. 

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mwaka huu 2025 limetangazwa na mtandao wa world Travel Awards  ( WTA) kuwa  kivutio bora cha utalii baranı Afrika ikiwa ni mara ya pili baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka 2023.



 

Prof. Nagu awafunda madaktari, ampongeza Mhe. Rais kwa maboresho makubwa ya afya.

July 11, 2025 Add Comment

Na John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia eneo la Afya, Prof. Tumaini Nagu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kote nchini kuendelea kuzingatia taaluma na kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni kusherekea mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika Sekta ya Afya Msingi yaliyofanywa na Serikali kwa kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan Kinara wa Nishati Safi ya kupikia Duniani , aungwe Mkono - Sangweni

July 11, 2025 Add Comment

WhatsApp%20Image%202025-07-11%20at%2009.41.55


WhatsApp%20Image%202025-07-11%20at%2009.41.54%20(2)

WhatsApp%20Image%202025-07-11%20at%2009.41.54%20(1)

WhatsApp%20Image%202025-07-11%20at%2009.41.54

WhatsApp%20Image%202025-07-11%20at%2009.41.53



  • Apongeza kasi ya Dkt. Biteko na Uongozi Menejimenti ya Nishati katika kufanikisha Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.
  • Amesifu juhudi za TANESCO  na REA katika kutekeleza  Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia.
  • Atoa Rai kwa Watanzania kuhamia kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia


Na Mwandishi Wetu,


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mh. Charles Sangweni ametoa Rai kwa Wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suhuhu Hassan katika Kampeni ya Kitaifa  ya kuhamia kwenye Nishati Safi ya Kupikia.

Rai hiyo imetolewa tarehe 09 Julai, 2025  na Mhe. Charles Sangweni alipotembelea Banda la TANESCO  katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-Salaam yanayoendelea jijini Dar-es-Salaam.

Amesema Tanzania tuna bahati kuwa, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jemedari Mkuu wa Majeshi ya nchi yetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye Kinara wa Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani.

Amesema, Wizara ya Nishati na Watanzania wote kiujumla, ni muhimu tuunge mkono juhudi zinazofanywa na Rais wetu katika kuhakikisha Watanzania wanahamia katika Nishati Safi ya Kupikia kwanza kwa  kuhakikisha tunapokea na tunaendana na Kauli Mbiu ya Nishati Safi ya Kupikia na kuunga mkono jitihada alizozianzisha.

Amesema, "kama Watendaji, tumefurahi kuona, wenzetu wa TANESCO wameunga Mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kuja na kampeni ya kuhamasisha  matumizi ya vyombo mbadala vya umeme vinavyotumia umeme kidogo na ambavyo vinahakikisha Nishati inayotumika kwa ngazi ya kawaida kabisa majumbani inakuwa ni  Nishati Safi." Ameeleza kwa hisia za kuvutiwa na hatua hiyo Mha. Sangweni.

Mha. Sangweni ameeleza zaidi kuwa, katika kutembelea Banda la TANESCO, ameona vitu vingi, ikianzia kwa REA  Usambazaji wa Umeme unavyofanyika kwa kasi na hii inaonyesha kuunga mkono Juhudi za Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine wa Wizara akiwemo  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko

Pia, Mha. Sangweni amesema vilevile katika Banda la TANESCO amekuta Wadau wanauza majiko ya umeme yanayotumia Nishati ya umeme kidogo sana ikilinganishwa na majiko mengine ya kawaida.

Mkurugenzi Mkuu wa PURA ameeleza  kufurahishwa kwake zaidi na  majiko hayo yanayotumia mfumo wa sumaku kupitisha moto  kuwa na mfumo wa ku-sence  pale ambapo sufuria haiko jikoni na namna yanavyopunguza kabisa upotevu wa umeme ambao hautumiki.

"Tumeona kwamba, usipoweka sufuria basi hakuna moto ambao unatoka na wakati mwingine ukiwa umejisahau, kunakuwa na timer ambayo inaweza ikazima jiko kulingana na jinsi ulivyo- set." Amesema Mha. Sangweni.

Amefafanua kuwa, hiyo yote ni katika kuhakikisha kwamba bili iliyokuwa inakuja kwa kiasi kikubwa ambayo ilikuwa inakuja kutokana na majiko ambayo hayana control kama hizo, inaenda kupungua kwa kiasi kikubwa sana.

"Hatua hiyo itatufanya sisi ambao vipato vyetu sio vikubwa kuona kuwa kutumia umeme sio anasa tena bali ni Matumizi Bora Kabisa ya Nishati ambayo iko safi na inayofaa kwa matumizi na ulinzi wa mazingira kama ambavyo Viongozi wetu wa nchi wamekuwa wakituhimiza na kusisitiza ili kama nchi tuingie kwenye Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia." Amesema Mha. Sangweni.