Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

RC BALOZI BATILDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAHIMIZE WAUMINI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

February 12, 2025 Add Comment


Na Oscar Assenga,Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amewaomba viongozi wa dini katika mahubiri yao wawahimize waumini kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha Kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwemo kuboresha taarifa zao.
Dkt Batilda aliyasema hayo Leo wakati akizungumza na viongozi wa dini na ya wa vyama vwanasiasa katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema zoezi la uboreshaji wa Daftari la kura litaanza February 13 mwaka huu mpaka 19.


Alisema ni upo umuhimu Makubwa viongozi hao kutumia majukwaa yao kuhakikisha wanawaelimisha waumini juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika zoezi hilo muhimu ili kupata haki ya  kuwachagua viongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
"Ndugu zangu viongozi wa dini naombeni mtumie mahubiri yenu kuhakikisha mnawahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura siku zimefika kesho tutakuwa na siku ya uandikishaji daftari "Alisema 
"Hivyo kupitia Tume Huru ya  uchaguzi walikuja na kufanya semina na viongozi wa vyama na mafunzo kwa wataalamu na Jumuiya ngazi za Kaya na Mawakala na kesho tunakwenda kwenye zoezi la uandikishaji wale vijana waliofika miaka 17 ambapo ikifika mwezi Octoba watafikisha miaka 18 wanapaswa kujitokeza kujiandikisha"Alisema




Mkuu huyo wa Mkoa alisema zoezi hilo litakwenda sambamba na la pili la  kuboresha taarifa na kusahihisha taarifa ambalo pia lina umuhimu hivyo wananchi wahakikishe wanachangamkia fursa za uwepo wa zoezi hilo.

KATIBU WA SUKI RABIA -KILICHOFANYWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU HAKIJAVUNJA KATIBA YA CHAMA

February 04, 2025 Add Comment

 NA WILLIUM PAUL, ROMBO.


MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid amesema kuwa kilichofanywa na Wajumbe wa Mkutano mkuu kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mwaka huu ni kwa mujibu wa katiba ya Chama.

Rabia ambaye ni mlezi wa Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro alitoa kauli hiyo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ambapo kimkoa yamefanyika kata ya Katangara mrere wilayani Rombo.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wkaipotosha kuwa kilichofanyika na Wajumbe hao ni kukiuka katiba ya chama na kuwataka wanaccm na wananchi kuwapuuza.

"Mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndio chombo cha mwisho cha maamuzi na kilichofanywa na Wajumbe wake kimezingatia katiba ya Chama hivyo wapuuzeni hao wanaoibuka na kutoa taarifa za uongo" Alisema Rabia.

Mjumbe huyo wa Nec alisema kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaenda kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 ili kuhakikisha wagombea wake wanashinda kwa kishindo na Tanzania inaenda kuwa ya kijani.

Alisema kuwa, kwa sasa wameshawahesabu wapiga kura wa ccm na uchaguzi wa mwaka huu Chama kitaenda kushinda kwa kishindo na kuwataka Wapinzani kukaa mkao wa kula.

Rabia alisema kuwa, hakuna chama chenye historia kama CCM na uimara wake ambapo wananchi wamekuwa wakikituma kupitia viongozi wake na wao wapo tayari kutumwa na kuwatumikia wananchi.

Aliongeza kuwa, Kilimanjaro imebadilika katika swala la umoja upo vizuri na hana shaka katika uchaguzi wa 2025 chama kitashinda kwa kishindo ili kukuza nguvu na umoja kama Watanzania.

"Wananchi mnawajibu wa kumuongezea moyo wa kutafuta fedha nyingi zaidi za maendeleo kwa kumpa kura nyingi za kishindo pamoja na kuilinda na kuitunza miradi inayotekelezwa ili iweze kudumu muda mrefu.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Seleman Mfinanga alisema kuwa, miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama hicho yapo mafanikio makubwa ya kujivunia katika kipindi chote hicho.

"Miaka 48 ya CCM tumeshuhudia ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali za elimu, Afya, Barabara, maji na hili ni jambo la kujivunia katika miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi" Alisema Mfinanga.










RAIS SAMIA AMEING'ARISHA CHAMWINO KIMAENDELEO -DKT BITEKO

February 02, 2025 Add Comment


📌Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 elimu ya Sekondari Chamwino


📌Uboreshaji wa miundombinu shilingi bilioni 17.9 zimetumika


📌Vijiji  vyote 47 Chamwino vimewashwa umeme


📌Asema Sekta ya Nishati ipo salama 


*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuing'arisha Chamwino kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo.


Hayo yamebainishwa leo Februari 02, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka 5, (2020  2025) iliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi. 


"Nimemsikiliza Mhe. Ndejembi akieleza kazi kubwa ambayo Serikali imeifanya hapa Chamwino, ni dhahiri kwamba Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Dkt. Samia imefanya kazi kubwa ya kuing'arisha  Chamwino na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hili. Hongereni sana, " Amesema Mhe. Biteko


Aidha, amewataka kuendelea kuisimamia Serikali kuanzia ngazi ya chini ili kuendelea  kuyagusa maisha ya wananchi kikamilifu na kutatua kero na changamoto walizonazo.

"Ni ukweli usiopingika kwamba Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana na ya kutukuka ya  kuiletea nchi yetu maendeleo. Ninyi hapa Chamwino ni mashahidi wakubwa wa maendeleo yaliyofanywa na Serikali chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan," ameongeza Dkt. Biteko.


Vile vile, Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 katika kugharimia elimu ya Sekondari tu katika Wilaya ya Chamwino.

"Tunashuhudia kuendelea kukamilika kwa ujenzi wa Shule hii ya Mkoa ya Sekondari ya ya Bweni ya Wasichana Manchali ambapo Watanzania wote watapata huduma za elimu," ameongeza Dkt. Biteko


Katika hatua nyingine amesema kuwa, uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga madaraja, vivuko na barabara za lami ndani ya Jimbo la Chamwino zaidi ya Shilingi bilioni 17.9 zimetumika.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaj, Adam Kimbisa amewahimiza wakazi wa Chamwino kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwao ili kulinda madanikio yaliyofikiwa.

Pia, amewata kutumiia mvua za msimu kulima kwa wingi na watakapopata mavuno wahifadhi sehemu ya mavuno yao ili kuwa na akiba ya chakula kwa siku zijazo. 


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa jitihada za Rais Samia kutoa fedha za miradi zimechangia kuharakisha maendeleo ya jimbo ikiwemo usambazaji wa nishati ya umeme kwa wananchi. 


"Kata zote 14 zenye vijiji 47 zimewashwa umeme ambapo kazi hiyo imefanyika katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024," amesema Mhe. Ndejembi.

KATIBU WA BAVICHA AKANA MADAI YA KUTUHUMIWA KUKIHUJUMU CHAMA

December 06, 2024 Add Comment





Na Oscar Assenga,TANGA.

KATIBU Mstaafu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Tanga (Bavicha) Hemed Said amekana madai ya viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya wanaomtuhumu kukihujumu chama wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika November 27, 2024.

Tuhuma hizo dhidi yake zinadaiwa ni baada ya Said kushiriki katika kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa wilayani Tanga ambapo Kwa pamoja walipongeza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa , vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe ambapo yeye alishiriki kama mgombea licha ya kuwa alienguliwa baada ya kukosa sifa ya kukidhi vigezo.



Akizungumza katika mkutano huo Said alisema kuna sintofahamu kwa chama hicho kumtuhumu kwamba anahusika moja kwa moja katika kuhujumu mipango ya chama jamba ambalo alilipinga kutokuhusika kutokana na kwa sasa amekwisha kustaafu na hawezi kuingia kwenye chama kwa njia yeyote bila kufuata taratibu za kichama"



" Kufuatilia kadhia hii nimekupa nikipata wasiwasi kwa sababu ninapata vitisho kwa baadhi ya wenzangu wakiwemo viongozi na wanachama changu kwamba ninahusika wakati siwezi kuhusika kwa namna yeyote ya kukihujumu chama hivyo naomba nijivue na sihusiki kwa sababu nipo ndani ya chama kwa zaidi ya miaka 15 nafahamu taratibu miongozi na kanuni zinazohusu uendeshaji wa chama" Alisema Said.



Alisema wakati alipokwenda kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa alikwenda kama mmoja wa wagombea ambaye alienguliwa kwa hiyo maoni aliyoyatoa ni kama mgombea aliyeenguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa .



“Sasa hapo mimi ninahusikaje na tuhuma za kuuza au kurubuni mipango au kukwamisha shughuli zozote za mafanikio ya chama changu" alihoji Said.

Aidha amesema kuwa licha ya kupokea vitisho kutoka kwa viongozi na wanachama wa chama hicho lakini hakukuwa na utaratibu wowote wa kichama ambao uliofuatwa ikiwemo kumuita kwa nia ya barua.

Kiongozi huyo Mstaafu wa Bavicha Mkoa wa Tanga amesema alishiriki kikamilifu mchakato mzima wa uchaguzi kujisaidia chama chake kusaidia kuwapatia wagombea ambao watakwenda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa , vitongoji na vijiji.

“Tofauti zozote zinazozungumzwa kwamba Mimi nimehusika kukirubuni chama hizo sio za kweli kwa sababu nimeshiriki ndani ya chama ngazi ya wilaya kutafuta wagombea na mimi nikiwa ni mgombea wa mtaa ambao ninaoishi sasa nahusikaje kukihujuma chama “Alihoji.

“Haiwezekani nasikia wengine wanasema nimenunuliwa sio kweli nina maisha yangu ninajiendesha kila mtu anafahamu kwa sababu nina uchumi wangu binafsi" alisisitiza mwanachama huyo.

Ameeleza kuwa Chadema wilaya ya Tanga kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji iliweza kusimamisha wagombea 50 lakini wapo 8 ambao walijitoa wakati mchakato huo ikiendelea licha ya kukidhi vigezo alihoji kuwa wamechukuliwa hatua gani tofauti na yeye ambaye aliyeenguliwa kikanuni.

"Ndani ya chama chetu katika halmashauri ya Jiji la Tanga ambayo tuna mitaa 181 tulikuwa na wagombea 50 lakini 8 katika hao tulikuwa na mawakala 182 , je kwanini hawa 8 na Mimi na Hawa ni nani amerubunika , kama walijitoa chama kimewachukulia hatua gani mpaka mimi nionekane kama ninahusika moja kwa moja? Alihoji.

Alieleza kuwa tangu alipojiunga na chama hicho akiwa shule ya Sekondari na baadye kupata nafasi ya uongozi wa Baraza la vijana Bavicha Mkoa wa Tanga na ni miongoni mwa vijana ambao walisimama imara kukitetea chama hicho hivyo kuhusishwa na tuhuma za kukihujumu chama chake inampa wakati mgumu.


“Chama kinafahamu kuwa katika vijana ambao walisimama na kupambana kwaajili ya kukisimamisha chama Mimi ni mmoja wapo kwa sababu Nina nafasi yangu kuanzia ngazi ya chuo nimehusika kwenye project nyingi mpaka kwenye ushindi wa ubunge ambao tulipata 2015." Alisema.

Kutokana na hali hiyo amesema kwamba atawaandikia barua viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kisha kupeleka nakala ngazi ya Taifa ili kidai haki yake kama mwanachama halali wa chama hicho.

Alisisitiza kuwa kila mwananchi anauhuru wa kujiunga na chama chochote na kuwa mwanasiasa ambaye anaweza kusimamia maslahi ya wananchi pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

"Kuchagua chama chochote cha siasa ni utashi wa mtu binafsi kwa sababu wakati ninajiunga na CHADEMA hakuna mtu ambaye alinilazimisha tupo katika harakati kwaajili ya kuwasaidia wananchi popote pale ambapo upo uweze kupaza   sauti ya wananchi isikike"Alisema 

RC AWAHAKIKISHIA USALAMA WAPIGA KURA

December 05, 2024 Add Comment



Na Paskal Mbunga,Tanga

WAPIGA kura katika uchaguzi wa serikali za mkoani Tanga wamehakikishiwa usalama wa kura zao na kwamba hawana haja ya kukaa vituoni mara baada ya kupiga kura.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian mara baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Raskazone Jijini Tanga ambapo aliwahakikishia wakazi wa mkoa huo usalama wakati wote wa zoezi.

Alisema kwamba kwamba hakuna haja ya kukaa vituoni baada ya kur a, isipokuwa kila mwananchi atakayepiga kura baada ya kumaliza aondoke na kurudi nyumbani wakisubiri matokeo yatakayotangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi.

Mkuu huyo wa mkoa alikuwa anajibu swali la mwandishi mmoja aliyetaka kujua kwamba baada ya kupiga kura je kuna uhakika gani wa usalama wa kura hizo ambapo alisema kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi wawe na imani na vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya usimamizi wa zoezi hilo.

Alisema kwamba mkoa wa Tanga una vituo vya kupigia kura 5460 na kwamba vituo vyote vimewekewa ulinzi na usalama ili watu wapige kura kwa uhuru bila kubuguziwa.

Katika siku hii muhimu kitaifa, viongozi mbalimbali wa kimkoa na taifa walikwenda katika maeneo waliyojiandikisha. Mwenyekiti wa CCM (M), Rajabu Abrahaman alikwenda kupiga kura yake wilayani Pangani,