
Na Paskal Mbunga,Tanga
WAPIGA kura katika uchaguzi wa serikali za mkoani Tanga wamehakikishiwa usalama wa kura zao na kwamba hawana haja ya kukaa vituoni mara baada ya kupiga kura.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian mara baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Raskazone Jijini Tanga ambapo aliwahakikishia wakazi wa mkoa huo usalama wakati wote wa zoezi.
Alisema kwamba kwamba hakuna haja ya kukaa vituoni baada ya kur a, isipokuwa kila mwananchi atakayepiga kura baada ya kumaliza aondoke na kurudi nyumbani wakisubiri matokeo yatakayotangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi.
Mkuu huyo wa mkoa alikuwa anajibu swali la mwandishi mmoja aliyetaka kujua kwamba baada ya kupiga kura je kuna uhakika gani wa usalama wa kura hizo ambapo alisema kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi wawe na imani na vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya usimamizi wa zoezi hilo.
Alisema kwamba mkoa wa Tanga una vituo vya kupigia kura 5460 na kwamba vituo vyote vimewekewa ulinzi na usalama ili watu wapige kura kwa uhuru bila kubuguziwa.
Katika siku hii muhimu kitaifa, viongozi mbalimbali wa kimkoa na taifa walikwenda katika maeneo waliyojiandikisha. Mwenyekiti wa CCM (M), Rajabu Abrahaman alikwenda kupiga kura yake wilayani Pangani,
EmoticonEmoticon