Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

TANESCO YASHINDA TENA TUZO ZA UBORA HUDUMA KWA WATEJA ZA CICM

March 30, 2025 Add Comment






📌Urahisi wa upatikanaji huduma kwa njia za kidigitali watajwa moja ya kigezo cha kushinda tuzo hiyo

📌MD Gissima aibuka kidedea kwa Kusimamia Maboresho yenye tija huduma kwa wateja Sekta ya Umma.

Shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya the ''Most improved Organization'' eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).

Tuzo hizo zimetolewa 28, Machi 2025 jijini Dar es Salaam ambapo Shirika limepata tuzo hiyo baada ya kufanya maboresho ya kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi Irene Gowelle amesema Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika ikiwa ni ishara nzuri ya maboresho yanayofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.

‘’ Tuzo hizi ni heshima kubwa kwa TANESCO, zinatuongezea ari ya kufanya vizuri zaidi,tutaongeza ubunifu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu’’






Aidha , Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga na yeye alishinda Tuzo ya heshima ya Kiongozi anayefanya mabadiliko chanya yenye tija upande wa huduma kwa wateja katika Sekta ya Umma.

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.





Wakazi Wanne wa Wilaya ya Same Wakamatwa kwa Kusafirisha Dawa za Kulevya

March 29, 2025 Add Comment
Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi jana tarehe 28 Machi 2025, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa jumla ya kilogramu 518.57.

ZAIDI YA WANANCHI 9,450 KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI WILAYA YA KOROGWE

March 29, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga, TANGA


ZAIDI ya Wananchi 9,450 wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya upatkanaji wa maji baada ya Serikali kuzindua mradi wa Kitaifa wa Ujenzi wa Visima 900 ambao unalenga kutatua changamoto hiyo.

Kati ya visima hiyo Mkoa wa Tanga watapata visima 53 ambavyo vitajengwa kila jimbo

Akizungumza mradi huo katika Kijiji cha Makorora wilaya Korogwe Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema kwamba visima 8 vimejengwa na kati ya hivyo vitano vimejengwa katika Jimbo la Korogwe Vijiji na Vitatu Korogwe mjini.

Alisema kwamba hatua hiyo ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wana watua ndoo kichwani wakina mama hapa nchini kwa kuwekwa huduma hiyo karibu na maeneo yao ili kuwaondolea adha ambazo walikuwa wanakumbana nazo awali.

“Leo hii tumekuja kushuhudia katika jimbo la Korogwe Visima vilivyochimbwa na hivyo yote ni kuhakikisha tunamtua Ndoo kichwani Mama kama ilivyo azma ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu tumefanya hivyo kuonyesha maji yamefika kwa wananchi”Alisema

Awali akizungumza Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema kwamba wataendelela kuboresha huduma za maji katika maeneo ya vijiji kwa kuendeleza miradi ya maji kila eneo ambalo halijaunganishwa na huduma hiyo

Alisema huduma hiyo iwafikie ndani ya muda mfupi ili waweze kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu na hivyo kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli nyengine za maendeleo.

Lengo la Serikali ni kuwapatia maji wananchi kwa asilimia 85 vijiji na aslimia 95 maeneo ya mijini





MARA WARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA

March 29, 2025 Add Comment


📌 Wamshukuru Rais Samia kwa kupunguza gharama za umeme


📌 Elimu kuhusu matumizi bora ya nishati yatolewa


📌 Watakiwa kuchangamkia fursa ya kuunganisha umeme


Wananchi mkoani Mara wamesisitiza kuridhishwa na utekelezaji miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inayotekelezwa nchini kwa lengo la kuwapatia umeme wa gharama nafuu, na wameipongeza Serikali kwa kuwafikishia miradi hiyo muhimu yenye faida kwa uchumi wa Taifa.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi kwa Wataalam wa REA waliofika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa katika Kata ya Kwangwa wilaya ya Musoma mkoani Mara. 


Aidha, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha REA kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani humo.


Awali Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomij ametoa elimu kwa umma kuhusu gharama za kuunganisha umeme, matumizi bora ya nishati, kuhamasisha kuunganisha umeme, tahadhari za umeme na elimu kuhusu utunzaji wa miundombinu ya umeme. 

Naye, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mara, Omary Gwillah, amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo ili wananchi wafanye shughuli zao kwa tija. 

Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kwangwa, Bwiso Kinanda, ameishukuru Serikali kwa kupunguza gharama za uvutaji umeme. Amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya uvutaji wa umeme. 

Vile vile, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwangwa B, Maxmilian Kunju akizungumza kwa niaba ya wananchi ameiomba REA kuendelea kufikisha umeme kwenye maeneo mengine mkoani humo ili wananchi wa Musoma wapate nishati ya umeme.


TANESCO YAANZA KAMPENI YA KUTOA ELIMU YA USALAMA KWENYE MATUMIZI YA UMEME MIKOA YA KANDA YA ZIWA

March 29, 2025 Add Comment


📌Kampeni inalenga kuelimisha watoto kuzingatia usalama kwanza watumiapo umeme. 


📌Itasaidia Kupunguza athari na ajali zitokanazo na majanga ya umeme kwenye Mikoa hiyo.

Shirika la Umeme Tanzania  (TANESCO) Machi 27 limeanza kampeni maalumu ya kuelimisha juu ya kuzingatia usalama kwanza kwenye matumizi ya Umeme kwa Makundi ya watoto katika shule mbalimbali za msingi zilizopo kwenye mikoa ya Mara, Kagera, Mwanza, Geita na Simiyu.

Kampeni hiyo inayoitwa " Zingatia Usalama Kwanza Utumiapo Umeme" inalenga kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na kuwapa elimu inayowawezesha kugundua vihatarishi vinavyoweza kusababisha ajali zinazotokana na majanga ya umeme na kuepuka  athari zitokanazo na majanga hayo.

Akizungumza katika moja ya Shule zilizotembelewa Kaimu Meneja Masoko kutoka TANESCO Bwana Sylvester Matiku amesema elimu hiyo ni muhimu kuwalinda watoto na majanga ya umeme kutokana na kuwa kati ya makundi yanayopata athari zaidi na ajali za umeme.

''Shirika limeona lianze kampeni hii hasa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na hivi karibuni kuwa na matukio ya ajali zitokanazo na umeme zinazoathiri zaidi watoto na hivyo tukaona tuje kuwaelimisha ili kusaidia kupunguza na kuondoa madhara ya ajali zitokanazo na umeme''.

Wanafunzi hao wamepatiwa elimu kuhusu Matumizi Sahihi ya Umeme ili kuokoa gharama pamoja na kuitambulisha namba mpya ya ya huduma kwa wateja bila malipo ya Mchongo 180.

Katika kampeni hiyo Wanafunzi katika  shule mbalimbali wamepata fursa ya kuhoji maswali kuhusu umeme na athari za umeme na jinsi ya kumsaidia muathirika wa ajali za umeme.

Wanafunzi hao wameahidi kufikisha elimu waliyoipata kuhusu Umeme na Usalama katika Kampeni ya hiyo kwa familia zao, ndugu, jamaa na marafiki na wameomba elimu hiyo pia ifikishwe kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum.

Kampeni hii muhimu inaendelea kwenye mikoa yote Kwenye Kanda ya Ziwa.