TCU YATANGAZA AWAMU YA PILI YA UDAHILI WA VYUO KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027

September 08, 2026

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa,akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 8,2026 jijini Dodoma  kuhusu kukamilika kwa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027/.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa,akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 8,2026 jijini Dodoma  kuhusu kukamilika kwa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027/.

Na.Alex Sonna-DODOMA 
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na programu za Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027 na kuanza kwa Awamu ya Pili ya udahili kuanzia leo, Septemba 8 hadi 21, mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Septemba 8,2026 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa, amesema jumla ya waombaji 149,645 waliwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo 93 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi wa Shahada ya Kwanza katika mwaka wa masomo 2026/2027.
Prof. Kihampa amesema katika mwaka huo wa masomo, vyuo vimeongeza programu za Shahada ya Kwanza kutoka 894 mwaka 2025/2026 hadi kufikia 1,019, sawa na ongezeko la programu 125, huku nafasi za udahili zikiongezeka kutoka 205,652 hadi 227,555.
Amesema ongezeko hilo la nafasi 21,903 ni sawa na asilimia 10.7, hatua inayolenga kuongeza fursa kwa vijana wanaohitaji kuendelea na elimu ya juu nchini.
Aidha, ameeleza kuwa katika Awamu ya Kwanza, waombaji 117,334, sawa na asilimia 78.4 ya waombaji wote, wamepata nafasi za udahili katika vyuo walivyoviomba, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka baada ya kukamilika kwa Awamu ya Pili.
 "Waombaji waliopata udahili katika vyuo zaidi ya kimoja wametakiwa kuthibitisha chuo kimojawapo kuanzia Septemba 8 hadi 21, 2026, kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kupitia ujumbe mfupi wa simu au barua pepe waliotumia wakati wa kuomba udahili."amesema Prof. Kihampa
Aidha, TCU imewataka waombaji ambao hawakupata nafasi katika Awamu ya Kwanza, pamoja na wale ambao hawakuweza kuwasilisha maombi, kutumia fursa ya Awamu ya Pili kwa kutuma maombi katika vyuo na programu wanazozipenda. Vyuo pia vimeelekezwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
"Tume imewakumbusha waombaji kuwa masuala yote yanayohusu udahili na uthibitisho wa nafasi yanapaswa kuwasilishwa moja kwa moja katika vyuo husika, huku vyuo vikielekezwa kushughulikia changamoto za waombaji kwa haraka kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya udahili," amesisitiza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »