NAIBU WAZIRI DKT. PIUS CHAYA ATEMBELEA KIWANDA CHA DAWA NCHINI CHINA

September 05, 2026


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya  ameanza ziara ya kikazi nchini China yenye lengo la kuvutia wawekezaji wa China kuwekeza nchini Tanzania. Dkt Chaya ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Balozi.Dkt. Batilda Buriani.


Katika kuanza kwa ziara hiyo leo, tarehe 5 Septemba 2026, Dkt. Chaya ametembelea kiwanda cha kutengeneza dawa cha Yiling Pharmaceutical Co., Ltd., ambapo amepata fursa ya kujifunza kuhusu shughuli za uzalishaji wa dawa na teknolojia zinazotumika katika kiwanda hicho.


Akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo, Dkt. Chaya amewaalika wawekezaji hao kuangalia fursa za kuwekeza nchini Tanzania, akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira na sera rafiki kwa wawekezaji, hususan katika sekta ya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.


Dkt. Chaya ameeleza kuwa Serikali, kupitia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, inalenga kuimarisha uzalishaji wa dawa na vifaa tiba nchini.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »