TRA KARIAKOO NA MABALOZI JENGO WAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUTOA ELIMU YA KODI KWA WALIPAKODI

August 21, 2026
Kariakoo, 20 Agosti, 2026

‎ Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo imeimarisha ushirikiano na uongozi wa Mabalozi Jengo kwa lengo la kuwafikia walipakodi na wadau mbalimbali kwa ufanisi zaidi.

Hayo yamejadiliwa katika kikao kazi kilichofanyika leo katika Ofisi za Gerezani-Kariakoo, ambapo pande zote zimejadili namna ya kutoa elimu ya kodi, kusikiliza changamoto za walipakodi na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari.

‎Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi, Bw. Khalid Mchuma, amepongeza uongozi wa Mabalozi Jengo kwa ushirikiano unaoendelea kuoneshwa kwa TRA, akieleza kuwa ni muhimu katika kuimarisha mahusiano na kuwafikia walipakodi kwa ufanisi.

‎Naye Mwenyekiti wa Mabalozi Jengo, Bw. Erasto Royemamu, ameeleza majukumu yao na kuwahimiza wamiliki wa majengo kufika TRA kwa ajili ya kupata ushauri wa kikodi, hususani wanapohitaji kuuza au kupangisha majengo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »