VISUKUKU MIMEA VYATOA MWANGA KATIKA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA NCHINI

July 02, 2026


Dar es Salaam

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu mchango wa sayansi ya visukuku mimea (Palynology) katika utafiti wa mafuta na gesi asilia kupitia Banda la TPDC kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).


Mtafiti Mwandamizi wa Visukuku Mimea wa TPDC, Bw. Johanes Kakoki, alisema uchambuzi wa visukuku mimea kama dinoflagellates ( viumbe vidogo sana vya majini aina ya planktoni) , chavua (pollen) na mbeguchembe (spores) husaidia kubaini umri wa miamba na uwezo wake wa kuzalisha na kuhifadhi mafuta au gesi asilia.


Aliongeza kuwa taarifa hizo huunganishwa na tafiti za kijiolojia, kijiofizikia na kijiokemia ili kuongeza usahihi wa kubaini maeneo yenye rasilimali za mafuta na gesi, huku teknolojia za kisasa zikiboresha ufanisi wa tafiti na kupunguza gharama.


Kupitia maonesho hayo, TPDC inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu hatua za utafiti wa mafuta na gesi asilia na mchango wa tafiti za kisayansi katika maendeleo ya sekta na uchumi wa Taifa.


*#Tunaboreshamaishanakuwezeshamaendeleo*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »