MTAKUWWA YAANZA OPERESHENI YA MALEZI BORA NA ULINZI WA WATOTO MWANZA

June 25, 2026


Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto Mkoa wa Mwanza (MTAKUWWA) imezindua kampeni ya “Amsha Ari” yenye lengo la kuhamasisha malezi bora, kuzuia mmomonyoko wa maadili na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Soko la Milongo, Mwenyekiti Mwenza wa MTAKUWWA Mkoa wa Mwanza, Yassin Ally, amesema kampeni hiyo itatekelezwa kwa mfumo wa nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na pango kwa pango ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Amesema baadhi ya maeneo hayo yamekuwa hatarishi kwa malezi ya watoto, hivyo kampeni hiyo imelenga kufikia makundi mbalimbali ya jamii kupitia mbinu tofauti za utoaji elimu na uhamasishaji.

Kwa upande wao, wajumbe wa MTAKUWWA Mkoa wa Mwanza ambao ni viongozi wa dini, wameitaka jamii, hususan waumini wao, kuzingatia malezi bora ya watoto na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara wa Soko la Milongo lililopo Kata ya Milongo, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameipongeza kampeni hiyo kwa kutoa elimu inayopinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuhamasisha jamii kuendelea kudumisha amani nchini




 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »