WAMILIKI WA VIWANDA VIPYA WATAKUWA KUAJIRI WAZAWA KUKUZA BIASHARA NA UCHUMI

May 10, 2026

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amewashauri Wamiliki wa Viwanda vipya Kutoa kipaumbele kwa wazawa katika ajira ili kukuza uchumi na mapato ya Taifa kwa ujumla.

Akizungumza Mei 09, 2026, wakati wa akifungua wa Kiwanda kipya cha kutengeneza tambi za papo hapo (Instant) cha Kura Food mkoani Pwani, amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara ikiwemo sera, miundombinu, na mifumo ili kuvutia Wawekezaji na wafanyabiashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania kimataifa.

Aidha, Wizara imefanya mapitio ya sheria na kanuni ili kuhakikisha zinajielekeza katika kuwezesha biashara na kuondoa vikwazo badala ya kudhibiti pekee. Lengo ni kushirikiana na wadau wa mnyororo wa thamani, kutumia teknolojia za kisasa zinazoongeza tija, uzalishaji, na ufanisi wa biashara nchini.

Naye, Mwenyekiti wa Kura Food, Bw. Wu Yeping, ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki yanayorahisisha uwekezaji,

Huku Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, akibainisha kuanza kwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara na Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia mwaka ujao ili kufungua zaidi fursa za kibiashara mkoani humo.

Naye Mbunge wa Kisarawe, Mhe. Selemani Jafo, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sera zake thabiti ambazo zimekuwa chachu ya kuvutia wawekezaji. Sera hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wananchi wa jimbo hilo kupitia kuanzishwa kwa viwanda vipya.

            

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »