KAFULILA: UJUMBE MAALUM SIKU YA MAMA DUNIANI.

May 10, 2026

Kupitia Ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa X (Zamani Twitter) Mwanasiasa na msomi wa masuala ya maendeleo, Mkurugenzi wa kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na binafsi (PPPC), David Kafuila ametoa ujumbe maalum wa maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani akisisitiza umuhimu wa malezi bora kwa watoto katika siku 1000 kuamzia kutungwa kwa mimba mpk umri wa 2 zina nafasi kubwa kubwa kuamua ubora wa watoto kiafya na zaidi kiakili.

Kafuila amesema kufikia Dira ya Maendeleo ya 2050, ubora wa rasilimali watu ndio msingi mkubwa wa maendeleo huku akieleza kuwa kipindi cha kuanzia mtoto akiwa tumboni hadi kufikisha miaka miwili kina mchango mkubwa katika afya na akili ya mtoto na ina nafasi kubwa kuzuia udumavu.

Amesema malezi na uwekezaji sahihi katika kipindi hicho vinaweza kusaidia kupunguza udumavu wa akili kwa watoto ambao bado ni changamoto katika bara la Afrika akinukuu tafiti za Benki ya Dunia zinazoonyesha kuwa uwekezaji sahihi kwa mtoto wa Afrika katika siku 1000 za mwanzo unaweza kuongeza zaidi ya dola trilioni 3.8 katika uchumi wa dunia ifikapo mwaka 2035 kupitia nguvu kazi yenye tija.

Aidha, amewapongeza akina mama kwa mchango wao mkubwa katika malezi ya familia na maendeleo ya jamii licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku.

Amehitimisha ujumbe wake kwa kuwatakia heri akina mama wote duniani, hususan mama wa Afrika wanaobeba jukumu kubwa la kulea na kukuza kizazi cha baadaye licha ya kupitia changamoto nyingi zinazotokana na kiasi na hali zao lakini zaidi na hali ya uchumi wa Afrika. HAPPY MOTHER'S DAY.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »