WATUMISHI PBPA WAHAMASISHWA KUPIMA AFYA NA KUPATA CHANJO YA HOMA YA INI

April 30, 2026

 

Daktari Johnson Katanga kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (OCR) amewahimiza watumishi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kujitokeza kupima afya zao na kupata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya *ugonjwa wa Homa ya Ini* (Hepatitis B).


Wito huo umetolewa leo wakati wa zoezi la utoaji elimu ya afya, upimaji wa hiari pamoja na utoaji wa chanjo dhidi ya *ugonjwa wa Hepatitis B* lililofanyika katika ukumbi wa PBPA jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika zoezi hilo, Dkt. Katanga alieleza kuwa chanjo ya Hepatitis B hutolewa kwa awamu tatu, ambapo dozi ya kwanza hutolewa *mara* baada ya mhusika kupimwa *na kuthibitika kuwa kuwa hana maambukizi* , dozi ya pili hutolewa baada ya mwezi mmoja, na dozi ya tatu hutolewa miezi sita tangu kupokea dozi ya kwanza.

Alifafanua kuwa chanjo hiyo ilianza kutolewa kwa watoto nchini tangu mwaka 2002 ikiwa sehemu ya chanjo za kawaida zinazotolewa mara baada ya kuzaliwa. Kutokana na hali hiyo, watu waliozaliwa mwaka 2001 na kurudi nyuma wanashauriwa kupata chanjo hiyo endapo hawajawahi kuipata.

Kuhusu dalili, Dkt. Katanga alisema *u* mgonjwa wa homa ya ini mara nyingi haoneshi dalili katika hatua za awali, hali inayosababisha watu wengi kugundua maambukizi wakiwa tayari wameathirika kwa kiwango kikubwa. Alitaja baadhi ya dalili zinazoweza kujitokeza baadaye kuwa ni pamoja na uchovu uliokithiri, maumivu ya tumbo upande wa juu kulia, *macho na ngozi kuwa na rangi ya njano* , kupoteza hamu ya kula, mkojo kuwa mweusi, kinyesi cheupe, pamoja na kuvimba kwa miguu au tumbo.

Aidha, alieleza kuwa maambukizi ya virusi hivyo yanaweza kutokea kupitia njia mbalimbali ikiwemo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, ~wakati wa kujifungua~ , kujamiiana bila kinga, kugusana na damu au majimaji ya mwili wa mtu mwenye ~yenye~ maambukizi, kushirikiana vitu vyenye ncha kali kama sindano, pamoja na kuongezewa damu iliyoathiriwa.

“Takwimu zinaonesha kuwa takribani watu milioni 254 duniani wanaishi na virusi vya homa ya ini, huku nchini Tanzania kiwango cha maambukizi kikikadiriwa kuwa asilimia 4. Hali hii ~Hii~ inaonesha umuhimu wa kuchukua hatua mapema,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa endapo maambukizi hayatagunduliwa mapema, kati ya asilimia 5 hadi 6 ya waathirika huingia katika hatua ya ugonjwa sugu (chronic), hali inayoweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo saratani ya ini.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Rasilimaliwatu~Utumishi~ wa PBPA, Bw. Matiko Sanawa, alisema kuwa utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kupitia Waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka ~2024~2014 unaosisitiza umuhimu wa kulinda afya za watumishi kazini.

Alisema mwajiri ana jukumu la kuhakikisha watumishi wanakuwa na afya njema ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuchangia maendeleo ya taifa.

“Tumewaalika wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kutoa elimu, kufanya upimaji wa hiari na kutoa chanjo. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha watumishi wanakuwa na afya bora,” alisema Bw. Sanawa.
Huu ni Mkakati wa Serikali wa kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza na ya kuambukiza, kwa kuhamasisha uchunguzi wa mapema na utoaji wa chanjo.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »