GASCO YATOA ELIMU YA USALAMA KAZINI, YAVUTIA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA OSHA

April 25, 2026
Watumishi wa GASCO katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya OSHA-mkoani Njombe

Kampuni ya Gesi Tanzania (GASCO), ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), inashiriki katika maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani (OSHA) yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali waliotembelea banda la GASCO, Muhandisi Vitus Augustino, ameeleza kuwa usalama na afya kazini si suala la kipaumbele tu kwa wafanyakazi, bali ni msingi muhimu waufanisi wa taasisi yoyote.

Amesema kuwa GASCO inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikishawafanyakazi wake wanafanya kazi katika mazingira salama, yenye kuzingatia ustawiwa kimwili, kisaikolojia na kijamii. “

Tunatambua kuwa mfanyakazi mwenye afya njema ya mwili na akili ana mchango mkubwa katika kuongeza tija na ufanisi wakazi. Ndiyo maana tunaendelea kutoa elimu na kuimarisha mifumo ya usalama kazini,” amesisitiza Bw. Augustino.
Muhandisi Vitus Augustino akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la GASCO


Aidha, amebainisha kuwa kupitia maonesho hayo, kampuni ya GASCO inalenga kuongeza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama naafya kazini, pamoja na kushirikiana na taasisi nyingine kubadilishana uzoefu na mbinu bora za kulinda wafanyakazi.


Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Mazingira bora ya kisaikolojia na kijamii kazini ni njia ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi nakujenga taasisi imara.” Kauli mbiu hiyo imelenga kuhamasisha waajiri na wafanyakazi kuzingatia si tu usalama wa kimwili, bali pia afya ya akili na mahusiano mazuri kazini.
Muhandisi Welignton Shango akitoa elimu kwa mwananchi aliyetemebelea banda la GASCO

Maonesho ya OSHA yamekuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za umma na binafsi, kwa lengo la kujadili na kuimarisha masuala ya usalama na afya mahali pa kazi nchini.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »