Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi leo Machi 03, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinazoshughulikia sekta ya mafuta na gesi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Mataragio, Kamishna wa Mafuta kutoka Wizara ya Nishati Goodluck Shirima, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA James Mwainyekule, Mtendaji Mkuu wa TPDC Mussa Makame Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Bruno Tarimo pamoja na wataalamu wengine kutoka wizarani na Taasisi hizo.
Kikao hicho kinalenga kuimarisha usimamizi, uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hizo ili kuimarisha sekta ya mafuta na gesi nchini.








EmoticonEmoticon