WAZIRI NDEJEMBI KUSHIRIKI KONGAMANO LA MAWAZIRI WA NISHATI WA AU NCHINI ETHIOPIA

December 09, 2025


📌*Kujadiliana mikakati ya kuendeleza matumizi bora ya Nishati*


📌*Mkakati na Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati barani Afrika kuzinduliwa*


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Disemba 09, 2025 amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Mawaziri wa Sekta ya Nishati wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuendeleza matumizi bora ya nishati kwa Bara la Afrika. 


Kongamano hilo litafanyika kwa siku mbili  ambapo nchi wanachama wa AU watabadilishana uzoefu katika mikakati, mipango, changamoto na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza ya miradi ya kuongeza ufanisi wa nishati katika bara la Afrika 

Katika kongamano hilo pia Mkakati na Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati barani Afrika utazinduliwa ambao unaendana na malengo ya Mpango wa Afrika wa Mwaka 1963. 


Aidha kongamano hilo la siku mbili limetanguliwa na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya Nishati katika kuwajengea uzoefu kwenye maeneo ya kupunguza Matumizi ya umeme katika sekta za majengo, viwanda, usafiri pamoja na majumbani.

Katika kongamano hilo Waziri Ndejembi ameongozana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.


Nchini Ethiopia Waziri Ndejembi amepokelewa na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Innocent Shiyo.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »