
Na Oscar Assenga, Tanga.
TAASISI ya Wazee Asili wa wilaya ya Tanga wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian kwa kusimamia vema amani na utulivu wakati wa mchakato wa uchaguzi na hivyo kupelekea kufanyika kwa amani na utulivu mkubwa.
Akizungumza niaba ya Taasisi hiyo Katibu Mkuu wake Mohamed Ali Dondo alisema kwamba amani na utulivu ambavyo vilitawala katika uchaguzi huo katika mkoa jambo ambalo limeonyesha namna kiongozi huyo wa mkoa pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama walivyoisimamia vizuri.
Alisema hatua hiyo imepelekea kuufanya mkoa huo kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi na hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani hapa nchini.
Katika hatua nyengine wamepongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ushindi mkubwa alioupta kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika hapa nchini siku ya Oktoba 29 mwaka huu, matokeo ambayo yameelezwa kuwa yameweza kudhihirisha mapenzi waliyonayo wananchi dhidi y Serikali yao.
Mbali na kumpongeza Rais huyo wa Jamhuri ya muungano pia alimpongeza makamu wa Rais Dkt Emmanuel Nchimbi na Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Aidha Dondo alisema,kwa ushindi huo alioupata Dkt Samia Suluhu Hassan wananchi wa Tanga wamejawa na imani kubwa juu ya kupata mabadiliko makubwa kwenye suala zima la kuharakishwa kwa maendeleo yao kupitia Serikali iliyoingia madarakani kupitia uchaguzi huo wa Oktoba 29 mwaka huu.
‘‘ Kwa niaba ya Tanga Asili tunamtakia maisha marefu na afya njema, tukiamini awamu hii kutakuwa na mabadiliko makubwa katika maendeleo ya wananchi’’ alisema Katibu Mkuu huyo wa Tanga Asili.
Kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo wa Tanga Asili, lengo la taasisi yao ni kuhakikisha kwamba wanarejesha hadhi ya Tanga kama ambavyo ilikuwa imeasisiwa na wazee wa nyakati zilizopita ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kwamba Tanga inakuwa salama wakati wote.
Mwisho.
EmoticonEmoticon