Kwa niaba ya Taasisi ya Tanzania Bloggers Network (TBN), ninatoa shukrani za dhati kwa Mratibu wa TBN Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Ndugu Cuthbert Kajuna kwa kazi nzuri na jitihada alizozionesha pamoja na muda mfupi wa taarifa ya kukusanya mabologa kuhudhuria mdahalo muhimu wa "Wajibu wa Kidijitali kwa Amani ya Nchi Kabla, Wakati na Baada ya Uchaguzi," ulioandaliwa na Jukwaa la Wachambuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Ushirikiano huu umeimarisha ushiriki wetru katika masuala ya kitaifa na hili ni la muhimu sana. Mwenyekiti wa TBN anathamini sana mchango huu mkubwa mratibu na wanachama walioacha shughuli zao na kufanya shughuli ya TBN, Mungu awabariki sana.
Beda Msimbe
Mwenyekiti TBN


EmoticonEmoticon