![]() |
Tume ya Madini inapenda kuwajulisha wadau wote wa sekta ya madini kuwa Maabara ya Tume ya Madini iliyopo Msasani, jijini Dar es Salaam, inaendelea kutoa huduma bora za kitaalam za upimaji na uthibitisho wa ubora wa madini kwa viwango vya kimataifa.
Kaimu Meneja wa Ukaguzi wa Madini na Huduma za Maabara, Mhandisi Mwarabu Mvunilwa, anawakaribisha wachimbaji, wafanyabiashara na wawekezaji wa madini kutumia huduma hizo ambazo zimeongeza ufanisi wa biashara ya madini na mapato ya Serikali.
Ameeleza kuwa Tume inaendelea kuboresha huduma hizo na kusogeza huduma karibu na maeneo ya migodi ili kuhakikisha wadau wanapata huduma kwa wakati, kwa gharama nafuu na ubora wa hali ya juu.
🔬 Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia:
📍 Ofisi: TIRDO Complex, Msasani, Dar es Salaam
📧 Barua Pepe: lab.coordinator@tumemadini.go.tz
📞 Simu: 0733 010 338
🌐 Tovuti: www.miningcommission.go.tz/laboratory



EmoticonEmoticon