MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi anatarajiwa kutikisa mkoani Pwani ambapo leo atafanya mkutano mkubwa wa hadhara.
Mkutano huo utakuwa wa kuhitimisha mikutano yake ya hadhara ya kampeni za kutafuta kura za ushindi wa kishindo wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani kwa mkoa wa Pwani.
Dkt.Nchimbi ataanza kufanya mkutano mdogo wa kwanza utaokafanyika katika eneo la Mlandizi, kisha baadae kulifunga pazia mkoa huo kwa mkutano mkubwa katika Wilaya ya Bagamoyo.
EmoticonEmoticon