Na Hamis Dambaya, DSM.
Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Abdul-Razaq Badru ametembelea maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa sabasaba na kupongeza kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya banda hilo Kamishna Badru amezipongeza taasisi hizo kwa kushinda tuzo nyingi zilizotolewa na mtandao wa World Travel Awards (WTA) by 28 Juni, 2025
Kamishna Badru amewaeleza waandishi wa habari kuwa sambamba na ushiriki wa Ngorongoro katika maonesho mbalimbali ili kujitangaza , pia mamlaka hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu ya utalii kama barabara, huduma za malipo, malazi kwa wageni na huduma za usafiri.
“Tumejipanga mwaka huu wa fedha kuhakikisha kuwa barabara zetu zinaboreshwa na kupitika muda wote, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jitihada zinaendelea kuongeza miundombinu ya malazi na huduma za usafiri ili kukidhi ongezeko la wageni wanaotembelea vivutio vyetu kila mwaka,”alisema Kamishna Badru.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inashiriki maonesho hayo ili kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kwa watembeleaji wa eneo hilo.
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mwaka huu 2025 limetangazwa na mtandao wa world Travel Awards ( WTA) kuwa kivutio bora cha utalii baranı Afrika ikiwa ni mara ya pili baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka 2023.
EmoticonEmoticon