DKT.YONAZI AIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU MAONESHO SABASABA

July 18, 2025


Na Mwandishi wetu- Dodoma


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya Taifa.


Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo tarehe 18 Julai, 2025 Ofisini kwake jijini Dodoma akikabidhiwa tuzo na  Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga iliyotolewa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025.



Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kupokea tuzo kumeongeza motisha katika ushiriki wa maonesho yajayo makubwa ya Kimataifa ya Sabasaba  na kutambua mchango wa Ofisi hiyo iliyoutoa kwa wananchi katika kipindi chote cha maonesho hayo na kutambua huduma ianayotolewa kwa wananchi.

“Ofisi ya Waziri Mkuu imefurahi sana kupokea tuzo hii kama ishara ya kutambua ushiriki wetu na mchango ambao Ofisi yetu inatoa kwa wananchi hivyo tunaamini ushiriki wetu unaofuata utakuwa wa viwango vya juu sana,” Alisema Dkt. Yonazi.



Pia  aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazofanya chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ndio mratibu wa Maonesho kwa  kuhakikisha maonesho hayo yanaleta tija na mageuzi makubwa katika sekta ya kiuchumi kwa wananchi na Kimataifa.


“Tunazishukuru sana Taasisi mbalimbali ambazo tumeshirikiana nazo na viongozi ambao wameendelea kutupa maelekezo yaliyowezesha kufanya vizuri katika maonesho hayo na tunaamini kwamba tutaendelea kuwa washindi au hata washindi wa jumla,”Alishukuru.

Ikumbukwe Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Sabasaba 2025 yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi tarehe 07 Julai, 2025 na kufungwa na Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa  katika viwanja vya maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 13, 2025.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »