Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Shule yake ya Biashara kimeandaa tukio la Siku ya Mzumbe na Kambi ya Wajasiriamali, litakalofanyika kwa mara ya kumi mfululizo katika Kampasi Kuu Morogoro, kuanzia Mei 6 hadi 8, 2026.
Akizungumzia kambi hiyo Meneja wa Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Mahusiano ya Kitasnia, Prof. Emmanuel Chao amewaalika wadau wote kushiriki katika Siku ya Mzumbe na Kambi ya Ujasiriamali 2026.
Kambi hiyo ya siku tatu inalenga kukuza ubunifu, ujasiriamali na kuwajengea uwezo wanafunzi pamoja na wadau wa biashara ili kukabiliana na changamoto za ajira, huku likitoa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.
Aidha, washiriki wanatarajiwa kujumuisha wanafunzi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo ya uchumi, ambapo kutakuwa na maonesho ya bidhaa na huduma, semina, warsha pamoja na majadiliano ya kitaalamu yanayolenga kuimarisha ujuzi wa vitendo na ushindani katika soko la ajira.


EmoticonEmoticon