DC KOROGWE AIPA KONGOLE MUHIMBILI NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION KWA HUDUMA ZA MATIBABU MKOANI TANGA

July 22, 2025


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema amekoshwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bure zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila kwa kushirikiana na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika kambi inayofanyika viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe mkoani Tanga.

 

Akizunguza katika kambi hiyo Mhe. Mwakilema amesema serikali inaendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya afya kwa kutambua umuhimu wa sekta hiyo kwa wananchi na namna inavyoweza kuchochea Uchumi wa nchi kwa kuwa jamii yenye afya madhubuti itakuwa imara katika shughuli mbalimbali za uwekezaji


“Nawapongeza sana Muhimbili na Vodacom Foundation Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboreshaji wa huduma za afya, wanaamini sana huduma za ubingwa bobezi zinazotolewa nanyi kutokana na historia na uwezo wenu wa muda mrefu hapa nchini ndio maana mnaona wamejitokeza kwa wingi” amebainisha mhe. Mwakilema. 


Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Watoto MNH. Dkt Aika Shoo amesema timu hiyo imejipanga kwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaofika katika kambi hiyo wanapata huduma bora kwa wakati bila gharama yeyote na hivyo amewaomba waendelee kujitokeza kwa wingi.


Naye Meneja wa Eneo -Vodacom Korogwe Bw. Kaanankira Nanyaro amesma Vodacom Tanzania Foundation wataendelea kushirikiana bega kwa bega na Muhimbili katika kuhakiisha kuwa wananchi wanapatiwa huduma za afya kadri itakavyowezekena.


MNH na Vodacom Tanzania wameanza kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bila malipo kuanzia Julai 21 hadi 23, kwa wakazi wa Tanga ambapo baadaye huduma hizo zitahamia katika Mkoa wa Kiliamjaro kuanzia Julai 25 hadi 27, 2025

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »