Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Kati ya fedha hizo, jumla ya shilingi Bilioni 4.450 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Kilimanjaro, ambayo tayari imeanza kufanya kazi huku ikiendelea na ukamilishaji wa maeneo yaliyosalia.
Kati ya fedha hizo jumla ya shilingi Milioni 352.509 zimetumika kukamilisha ujenzi wa Miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa, Ofisi 3 za walimu na matundu 3 ya vyoo vya walimu, Shilingi milioni 65.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu ya vyumba vitatu, Shilingi milioni 61.370 zikiwa zimetumika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya afya (Sick Bay), Shilingi milioni 194.067 zimetumika kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala sambamba na shilingi Milioni 104.640 zikitumika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu ya moja kwa mbili (2 in 1).
Shilingi Milioni 225.069 zimetumika kukamilisha ujenzi wa vyumba 4 vya maabara ya Fizikia, Baiolojia, Kemia na Jiografia. Shilingi milioni 50.871 zimetumika kukamilisha ujenzi wa matundu 16 ya vyoo sambamba na shilingi Bilioni 1.101 zikitumika kukamilisha ujenzi wa mabweni 8, Shilingi Bilioni 1.092 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo, Shilingi milioni 7.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wa vichomea taka viwili pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa mashimo 9 ya maji taka kwa gharama ya shilingi milioni 59.631
Sambamba na fedha hizo pia katika awamu ya pili ya mradi wa SEQUIP serikali imetoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa 10, Mabweni 4, nyumba za walimu 3, Chumba cha TEHAMA na Maktaba.
Wakati huo huo serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya Amali ya inayojengwa katika kijiji cha Roseline kata ya Ndumeti katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Ujenzi wa mradi huu upo katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, Maktaba na jengo la utawala, Maabara ya Kemia na Baiolojia pamoja na chumba cha TEHAMA, Ujenzi wa choo cha matundu 8 na mabweni matatu, Ujenzi wa Karakana ya uashi na umeme, sambamba na Bwalo la chakula na nyumba ya mwalimu.



EmoticonEmoticon