TRA SC YATWAA KOMBE LA DSSL MARA YA PILI MFULULIZO ,SASA MABINGWA WA KIHISTORIA

April 06, 2025


Na Mwandishi Wetu, Dar.


TIMU ya Mpira wa miguu ya Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ya TRA SC imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa kombe la Mashindano ya Wafanyakazi Dar Es Salaam 'Dar Es Salaam Staff Sports League' (DSSL) kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) waliokubali kichapo cha bao moja bila.

Mchezo huo wa fainali wa aina yake umrchezwa katika uwanja wa TRA Kurasini,  Aprili 5, 2025 ulishuhudiwa na shamrashamra na shangwe mbalimbali kwa mashabiki wa timu zote mbili ulikuwa wa kuvutia licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha dakika 45 za kwanza za mchezo huo,



Hata hivyo TRA SC walifanikiwa kupata bao kipindi cha pili, na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo, na kuwafanya kuwa mabingwa wapya wa kihistoria kwa kutwaa mfululizo, wakifanya hivyo mwaka jana 2024, na mwaka huu 2025.

TRA pia wameweza kuweka rekodi ya kipekee kwa upande wa timu ya Wanawake ya mchezo wa Netball waliweza kutwaa ubingwa dhidi ya Timu ya Wanawake ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), na kufanya TRA kuwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.

 Awali akikabidhi zawadi za ushindi, Mdau wa Michezo na Mwanamichezo nchini Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya  Michezo- Malya, Dkt. Jonas Tiboroha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Michezo BMT, alipongeza vipaji vya wachezaji wa timu zote huku akiomba maafisa Uajili kuendelea kuwekeza zaidi michezoni kwani inasaidia Wafanyakazi kuwa vyema kiafya na ufanisi kazini.



"Niwapongeze viongozi wa timu zote bahati nzuri mpo hapa.

Michezo inasaidia ufanisi, inapunguza hata bajeti ya matibabu, tuendelee kuwekeza kwenye michezo na tuangalie namna ya kuweka sawa Miundombinu ya michezo." Amesema Dkt  Toboroha na kuipongeza TRA kwa ujenzi wa uwanja huo wa kurasini hali inayowapa ufanisi mkubwa kwa kushinda makombe katika michuano mbalimbali ikiwemo SHIMUTA na mingine mingi ya Wafanyakazi nchini.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ligi hiyo, Japhari Saidi Mtoro amezipongeza timu zote kwa hatua waliofikia, huku akiahidi msimu ujao mambo makubwa.



"Mashindano ya wafanyakazi lazima yalindwe kwa nguvu na wivu mkubwa, hivyo ni muhimu kuwekeza katika mifumo itakayozuia mtu yeyote asiye na sifa kushiriki mashindano hayo. 



Akifafanua zaidi Mwenyekiti amesema kuanzia msimu unaokuja wataweka mfumo wa biometric utakaotumika kuwasajili na kuwatambua wachezaji kwa sura zao na alama za vidole.


Mashindano hayo yalishirikisha timu 14, zilizocheza mfumo wa Ligi, kila wiki ilikujenga Afya ya Watumishi wachezaji maofisini lakini pia kujiandaa na michezo mbalimbali pahala pa kazi.



MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng