SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR AANZA ZIARA YA SIKU NNE TANGA

April 24, 2025


Spika wa Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid, ameanza ziara ya siku nne mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akiwasili mkoani humo, Spika Zubeir alipokelewa kwa heshima na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurahman, na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dastan Kitandula.

Katika ziara hiyo, Mhe. Zubeir anatarajiwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo zikiwemo Handeni, Pangani, Mkinga, Muheza pamoja na jiji la Tanga. Aidha, atashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo ukaguzi wa miradi, uwekaji wa mawe ya msingi, pamoja na kukutana na wananchi na viongozi wa maeneo husika.


Ziara hiyo inalenga kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuendeleza ushirikiano baina ya pande mbili za Muungano, na kuangazia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.



Share this

Related Posts

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng