Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Jimbo la Mkinga Mhe. Dunstan Kitandula Leo ameshiriki mapokezi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Zubeir Ali Maulid. Mhe. Spika Atakuwepo Mkoani Tanga kuanzia tarehe 24-27 Aprili 2025.
Mhe. Maulid yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kuadhimisha sherehe za miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo pia atakagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuonyesha mafanikio ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sherehe za Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwaka huu inasherehekewa kwa viongozi wa kuu wa Nchi kufanya ziara mikoani kwa kufanya Shughuli mbalimbali ikiwemo ukaguzi na uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo.
EmoticonEmoticon