Fundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akiendelea na ujenzi wa tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

Fundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India akisuka nondo wakati wa ujenzi wa tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) kwenye Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na Wizara ya Maji eneo la Chamwino jijini Dodoma leo Machi 25, 2025 ambao Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ni wanufaika wa mradi huo ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.

Ujenzi wa Mradi wa Miji 28 Chamwino, Mkoa wa Dodoma unaendelea ambapo visima 8 vitakavyopeleka maji kwenye tanki la kuvunia maji vimekamilika.
Kazi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi wa matanki mawili ya lita laki mbili (200,000) eneo la Msanga, tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) katika eneo la Chamwino na ujenzi wa kituo cha kusukumia maji eneo la Chamwino.
Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi MEGHA Engineering &Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.
Mradi huu unatekelezwa chini ya Wizara ya Maji ambapo Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ni miongoni mwa wanufaika katika kanda yake ya Chamwino.
Akizungumza leo Jumatatu, Machi 24, 2025 Kaimu Meneja wa Chamwino, Gray Mbalikila amesema Mji wa Chamwino unakua kwakasi, hivyo kupitia mradi huu hali ya maji itaimarika zaidi na kuweza kusogeza huduma maeneo ya pembezoni ambayo yanakua kwa kasi zaidi kwasababu uzalishaji wa maji utaongezeka na miundombinu ya mabomba itaboreshwa zaidi.
“Mradi huu unahusisha kazi ya uchimbaji na uendelezaji wa visima virefu ambavyo vinapatikana katika eneo la bonde la maji la Chamwino, ujenzi wa tanki la kuvunia maji katika eneo la Chamwino lenye ujazo wa lita lakitano. Tanki hili litakusanya maji kutoka kwenye visima virefu 8," amesema Mbalikila
Pia ujenzi wa kituo kikuu cha kusukumia maji kwenda katika tanki la Buigiri lenye ujazo wa lita milioni mbili na laki tano (2,500,000) na tanki la juu lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga.
Kazi nyingine ni usambazaji wa maji kwenda katika eneo la huduma ya kitokea kwenye tanki la Buigiri kwa bomba kubwa kwenda katika maeneo ya Buigiri, Chinangali II, Mwegamile na Chamwino na usambazaji wa maji kutoka kwenye tanki la Msanga kwenda katika maeneo ya Msanga
Halima Kambi
Ass. Communication OfficerDodoma Urban Water Supply and Sanitation Authority (DUWASA)P.O. BOX 431 Dodoma
Mobile; 0655 729791/ 0785 303969
DODOMA
Ass. Communication OfficerDodoma Urban Water Supply and Sanitation Authority (DUWASA)P.O. BOX 431 Dodoma
Mobile; 0655 729791/ 0785 303969
DODOMA
EmoticonEmoticon