📌Shirika labeba tuzo 4 kati ya 12 zilizoandaliwa.
📌Mawasiliano ya Kimkakati na Ubunifu vyatajwa kati ya sababu za Ushindi huo.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kung'ara baada ya kushinda jumla ya tuzo 4 kati ya 12 zilizotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania(PRST)kwa mwaka 2024.
Tuzo hizo zilizotolewa 29, Machi 2025 jijini Dar es Salaam zililenga kutambua mchango wa Idara za Uhusiano na Mawasiliano za Sekta ya Umma na binafsi ambazo zimekua mstari wa mbele na mahiri katika mawasiliano ya kimkakati.
TANESCO imeibuka mshindi wa kwanza kwenye vipengele vya "Best Digital PR Campaign" kupitia kampeni yake maboresho ya mita za LUKU (TID) ya ''Mita yako tuna kazi nayo'' (TID)iliyofanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii.
Kipengele cha ''Best PR Department of the year 2024" iliyotokana na Muundo na utendaji bora wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Shirika.
Imeshinda pia kipengele cha ''Best Crisis and Communication Plan and Strategy" kutokana na Kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara zinapotokea changamoto kuwa wepesi kutoa taarifa,ufafanuzi wa haraka na mawasiliano ya kimkakati.
Mbali Mafanikio hayo ya Kitaasisi Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Irene Gowelle ameibuka Mshindi wa Tuzo ya "Tanzania PR Golden Star of the Year" kwa mchango wake katika kusimamia mawasiliano ya kimkakati na ubunifu katika kuwasiliana na Umma.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi Irene Gowelle alieleza kuwa tuzo hizo ni heshima kubwa kwa Shirika ikiwa ni ishara ya kutambulika kwa kazi kubwa zinazofanyika katika mawasiliano kwa umma na juhudi kubwa ya Kurugenzi katika kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
‘’Tuzo hizi ni kubwa sana kwa TANESCO, tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuwasiliana na Watanzania ili kujenga taswira nzuri ya Shirika letu na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi,alifafanua Bi Irene.
Vilevile ameushukuru uongozi wa Wizara ya Nishati,Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika kufanikisha shughuli mbalimbali ndani ya Kurugenzi ya Mawasiliano hatua ambayo imechangia kazi za mawasiliano zinazofanyika kuonekana na kutambulika kwa jamii.
"Napenda nichukue nafasi hii kuushukuru Uongozi wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO kwa ushirikiano mkubwa ambao unatuwezesha na kutupa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu kwa weledi na ufanisi mkubwa"
Kwa upande wake Rais wa PRST Bw. Assah Mwambene, alisema utoaji wa tuzo hizo ni kutambua na kuthamini kazi za idara za mawasiliano za Sekta ya Umma na Binafsi ili kuboresha utoaji wa huduma katika maeneo yao.
Tuzo za PRST zinalenga kutambua mchango wa mafanikio ya mawasiliano ya kimkakati katika sekta ya umma na binafsi nchini ambapo TANESCO imeonesha umahiri wake katika sekta ya mawasiliano ya kimkakati kwa mwaka 2024.
EmoticonEmoticon