![]() |
📌Mitungi 26,040 kusambazwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Tanga |
📌Mitungi 3,255 kusambazwa kwa bei ya ruzuku wilaya ya Korogwe
📌Majiko ya gesi ni nishati safi na salama ya kupikia yenye kutunza mazingira na rafiki kwa afya ya watumiaji
REA imeendelea na zoezi la usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya Korogwe.
Ukiwa ni muendelezo wa uhamasishaji na upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia vijijini pamoja na maeneo yaliyo pembezoni mwa miji.
Gharama ya mradi ni milioni 455.7 na mwanachi atatakiwa kuwa na kitambulisho chake cha Taifa (NIDA) pamoja na pesa taslimu 17,500 tu.
Mitungi inapatikana kwa gharama nafuu, yanatunza mazingira, yanadumu na rafiki kwa afya ya watumiaji.
EmoticonEmoticon