MKURUGENZI UFUATILIAJI NA TATHIMINi WIZARA YA NISHATI AELEZA JINSI WIZARA INAVYOTOA FURSA KWA WANAWAKE

March 01, 2025


Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Nishati, Bi. Anita Ishengoma amesema katika utekelezaji wa majukumu ya kisekta Wizara ya Nishati imetoa fursa za usawa kwa wanawake.


Bi. Ishengoma ameyasema hayo katika  kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 Machi ambapo nchini itaadhimishwa kitaifa mkoani Arusha.


"Usawa hapa wizarani unazingatiwa kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wanawake katika ngazi ya maamuzi ambayo inafikia 5." Amesema Bi. Ishengoma

Amesema kuwa uwepo wa uwiano wa jinsia unatoa fursa sawa kwenye maamuzi katika ngazi za juu katika kutekeleza majukumu ya ki sekta. 


 Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ameasa Wanawake kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »