Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Mhe. Kakunda ameipongeza Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Serikali kwa ujumla kwa kubuni, kuanzisha na kutekeleza Miradi mbalimbali ya kusambaza nishati ya umeme kwa Wananchi wa mkoa wa Singida na kuongeza kuwa umeme ni fursa ya kuboresha maisha ya Watu vijijini kama utatumika ipasavyo.
![]() |
“Tumefurahishwa na tuliyoyaona hapa katika kijiji cha Kitopeni; Aghondi na kwenye zahanati ya kijiji cha Mabondeni. Tunaishukuru Serikali kupitia REA kwa udhibitisho wa uwepo wa umeme. Tunatoa wito kwa Wananchi, kasi ya kujiunganisha na huduma ya umeme, iongezeke; wekeni mpango ili kuhakikisha umeme unawasaidia kujiletea maendeleo yenu.” Amesema, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Mhe. Kakunda.
![]() |
Katika taarifa yake mbele ya Kamati ya PAC; Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti Bwana Godfrey Chibulunje ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA; amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imetoa jumla ya shilingi bilioni 86.8 ili kuhakikisha Miradi minne (4) inatekelezwa mkoani humo ili kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na huduma ya umeme ili kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Wakala wa Nishati Vijijni (REA) unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi.”amesema Bwana Godfrey Chibulunje.
Kamati ya PAC ipo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo ambapo inatarajia kufanya ziara hiyo katika mkoa wa Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
MWISHO!!!
EmoticonEmoticon