UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI UMEKAMILIKA ASILIMIA 100

February 24, 2025


Ujenzi wa jengo la kisasa la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli umekamilika kwa asilimia 100 na leo Jumatatu Februari 24, 2025 limezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Jengo hilo linalenga kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma kwa wananchi.

Jengo hilo, lililojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 6, lina vyumba 72 vitakavyotumika na watumishi wa serikali na wakuu wa idara za Halmashauri ya Bumbuli, hivyo kutoa nafasi nzuri ya kuimarisha utendaji kazi wa serikali katika kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka na ufanisi.


Miundombinu ya jengo hili ni ya kisasa na imezingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalumu.


Kumbi kubwa na ndogo za mikutano za kisasa zilizopo katika jengo hili zitatoa fursa nzuri kwa viongozi na wananchi kufanya majadiliano na mikutano.

 Pia, mifumo ya maji safi na maji taka iliyowekwa katika jengo hili itahakikisha usafi na afya kwa watumishi na wananchi wanaohudumiwa, na hivyo kuchangia katika ustawi wa mazingira.

Mbali na hayo, jengo hili limezingatia pia mahitaji ya watu wenye ulemavu. Kwa kuwekwa kwa ngazi mlalo na vyoo maalumu.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »