📌 *Serikali yafuatilia kwa karibu upatikanaji umeme Lushoto*
📌 *Vijiji vyote Nkasi vyafikiwa na huduma ya umeme*
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema ni azma ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika na unaotabirika kwa ajili ya shughuli za kijamii na kimaendeleo.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Januari 03, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Lushoto Mhe. Shabani Shekilindi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaondoa changamoto ya kukatika umeme katika Wilaya ya Lushoto kwa kuweka suluhisho la kudumu.
"Tutafuatilia kwa hii wiki moja kufahamu ni nini changamoto ya kukatika kwa umeme Wilaya ya Lushoto, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge iwapo kuna matengenezo tutahakikisha yanakamilika kwa haraka." Amesisitiza Mhe. Kapinga
Akijibu swali Mbunge wa Nkasi Kusini, Mhe. Vicent Mbogo aliyetaka kufahamu uwepo wa nishati ya umeme katika Kijiji cha Msamba-Masokolo, Lyapinda, Izinga na Lyele na katika Vitongoji vya Kisenga na Lupata, Mhe. Kapinga amesema Wilaya ya Nkasi ina jumla ya vijiji 90 ambapo vyote vimepatiwa huduma ya umeme vikiwemo vijiji vya Lyele na Lyapinda.
Aidha, amesema Kitongoji cha Lupata kilichopo katika Kijiji cha Lyapinda kitapata umeme kupitia mradi wa Vitongoji 15 vya Mbunge utakaotekelezwa na Mkandarasi aitwae M/s STEG International Services Ltd ambaye ameshakamilisha hatua za upimaji na usanifu.
Ameongeza kuwa, uhakiki wa Kitongoji cha Kisenga umekamilika na Kitongoji hicho kitapatiwa umeme kupitia mradi wa vitongoji (HEP IIB).
EmoticonEmoticon