Na Paskal Mbunga, Tanga.
WIZARA ya Madini inakusudia kuipigia chapuo zoezi la uundwaji wa Bodi ya Wanajiolojia Tanzania (TGS) lengo likiwa ni kukiwezesha kuwa na chombo ambacho kitawaunganisha wataalamu hao watakaokwenda kuleta mabadiliko makubwa.
Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Msafiri Mbibo wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalamu wa wanajiolojia ambao ulishirikisha wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jijini Tanga.
Msimamo huo unatokana na kauli iliyotolewa kwenye mkutano huo na Rais wa Jumuiya wa Wanajiolojia Tanzania Dkt Elisante Mshiu aliposema kwamba kama taasisi hiyo haitopata bodi basi kinaweza kuwa kikwazo katika mchango wao katika kutimiza maono ya 2030.
.jpg)
Alisema kwamba wamelipokea wapo pamoja na wataendelea kuwasiliana kuona jinsi ambavyo wanaweza kuharakisha uundwaji wa bodi hiyo ili kuchochea kasi ya ukuaji wa chombo chenu.
“Wizara ya madini imeendelea kutumia wanajiosayansi katika kufanya tafiti kwa lengo la kubaini uwepo wa madini nchini kupitia maono ya Vision 2030 madini ni maisha,madini ni utajiri ni lengo la wizara ya madini na maono ya mheshimiwa Waziri kuhakikisha kwamba maisha ya watanzania yanabadilishwa kutokana na rasilimali hizi ambazo ni za thamani sana zilizopo Nchini,”alibainisha Katibu Mkuu.
‘Ili kufanikisha maono haya wanajiosayansi wameendelea kutumia utaalamu wao kkatika kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa lengo la kutambua tabia za miamba utambuzi huu unatuwezesha kufanyika kwa tafiti nyingine za jiosayansi zenye kuwezesha kubaini aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini,”alisisitiza Katibu Mkuu huyo.
.jpg)
Kwa upande wake Rais wa jumuiya ya wanajiolojia Tanzania Dkt. Elisante Mshiu amesema kwamba wamekutana kwajili ya kujadiliana juu ya mabadiliko kutoka kwenye nishati chafuzi kwenda kwenye nishati salama ambazo zote ukiangalia ni malengo ya serikali.
Amewataka wanajiolijio kuelewa majukumu yao hususani katika kuelekea kwenye maono ya 2030 huku akieleza kwamba bila kuwa na bodi ya usajili ya wanajiosayansi maono ya 2030 yanaweza kuwa na changamoto hivyo ameendelea kusisitiza umuhimu wa uundwaji bodi hiyo.
(mwisho)
EmoticonEmoticon