Meneja Huduma za Sheria wa Bohari ya Dawa (MSD), Elisamehe Macha (katikati) akizungumza na Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo ambao ni wateja wa MSD wakati wa ziara iliyofanyika Septemba 3, 2024. Kutoka kushoto ni Meneja wa MSD Kanda ya Tanga, Sitti Abrahman na kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi.
.....................................
Na Mwandishi Wetu, Tanga
WATEJA wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga wameipongeza MSD kwa maboresho makubwa wanayoendelea kuyafanya ya usambazaji wa bidhaa za afya na dawa kwa wakati.
Pongezi hizo
wamezitoa kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya
MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD kanda
hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi anayoifanya mkoani humo ya kuzungumza na wateja wanaowahudumia
ili kupata maoni yao juu ya maboresho ya shughuli za MSD na kupokea changamoto
zao ili ziweze kufanyiwa kazi.
Ziara hiyo
inafanyika ikiwa ni moja ya matukio ya kuadhimisha miaka 30 ya ufanyaji kazi wa MSD tangu ilipoundwa wakati huo ikiitwa Central Medical Store (CMS)
Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo),
Kibwana Mgude alipongeza MSD kwa kuwafikishia dawa kwa wakati na kueleza kuwa sasa
upatikanaji wa bidhaa za afya umeboreshwa kwa kiwango cha juu.
“ Sasa hivi tunapokea dawa na vifaa tiba kwa
wakati tunakila sababu ya kupongeza maboresho haya ya MSD,” alisema Mgude.
Kwa upande wake Magdalena Chambo ambaye ni
Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba alisema utaratibu unaofanywa na MSD wa
kuwapelekea bidhaa za afya ni mzuri tofauti na hapo nyuma ambapo walikuwa
wakipelekewa dawa hata zile ambazo walikuwa hawajaziomba.
Dkt. Mwifunyi akizungumza wakati wa ziara hiyo
alipongeza MSD kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba
kudumisha ushirikiano baina yao na wateja wao wanaowahudumia.
Dkt. Mwifunyi aliwasisitiza wateja hao wa MSD
kutoa mapendekezo yao ambayo wataona yana tija kwa ajili ya kuboresha shughuli
zinazofanywa na MSD.
“ Utoaji wa huduma bora za usambaji wa vifaa
tiba na dawa ni jambo jema kwani jamii na taifa wanatutegemea,” alisema Dkt.
Mwifunyi.
Katika ziara hiyo Dkt. Mwifunyi aliongozana na
baadhi ya maofisa wa MSD kutoka Kanda ya Tanga na Makao Makuu wakiongozwa na
Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha.
Kikao cha MSD na wateja wao Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kikiendelea
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Safari ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Hospitali ikifanyika.
Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo), Kibwana Mgude (kushoto) akitoa maelezo ya jinsi ya uhifadhi wa bidhaa za afya katika Hospitali hiyo.
Hapa wakipata maelezo katika chumba cha watu wenye changamoto ya magonjwa ya kinywa.
Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba, Magdalena Chambo (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Nkumba, Magdalena Chambo.
Mguu na njia wakati wa kwenda kutembelea baadhi ya idara za Hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo) wakati wa ziara hiyo.
EmoticonEmoticon