Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza Mkutano wa dharura wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi hiyo uliofanyika katika Afisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mjini Unguja, Zanzibar leo tarehe 11 Desemba, 2024.
Wakati wa Mkutano huo, Makatibu Wakuu wamejadiliana kuhusu suala la bajeti ya Misheni ya Ulinzi wa Amani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC) kwa mwaka 2024 hadi 2025.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Mhe. Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mhe. Amina K. Shaaban, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Talha Mohamed pamoja na maafisa waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
EmoticonEmoticon